Wahenga wanakuambia raha jipe mwenyewe, kama ulikuwa hujacheka tangu kumekucha basi hii itakupa tabasamu, ni baba na mwana ndani ya gari taratiibu wakiendelea na safari yao.
Kuna utamaduni wa watu wengi wanapokuwa safarini kujienjoy na muziki, hata kama safari ikiwa ndefu burudani ya muziki husaidia kupunguza uchovu na kuiona safari ni fupi.
Video hii toka Marekani inaonyesha baba na mwana wakijiachia na ‘let it go‘ yaFrozen hawa walijiachia na mzuka ulipanda zaidi, mikono ilikuwa juu muda wote huku wakiimba kwa sauti kubwa mwanzo mpaka mwisho.
Unaweza kutazama video ya baba huyo Billy akiwa na mtoto wake Blakely wakijiachia huku pembeni akiwa amekaa mwanamke mmoja ambaye hajaonekana vizuri, huenda ikawa ndio mke wa jamaa huyu.