Msikiti washambuliwa Sweden


Msikiti ulioshambuliwa nchini Sweden
Polisi nchini Sweden wanamtafuta mshukiwa mmoja katika kile ambacho wanamini kuwa shambulizi jengine kwenye msikiti likiwa ni la tatu wiki hii.
Bomu la petroli linaripotiwa kurushwa katika kituo nyumba hiyo ya ibada kwenye mji ulio masharikini wa Uppsala.
Hata hivyo jengo hilo halikushika moto.
Mapema wiki hii serikali ya Sweden ilichukua tahadhari maalum za kulinda misikiti baada ya vituo viwili vya maombi kuharibiwa na moto.