Mmoja wa watu waliopanga mashambuliz ya kigaidi kwenye balozi za marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 ameaga dunia kabla ya kufikishwa kizimbani mjini New York.
Wakili wa Abu Anas al-Liby amesema kuwa afya ya mshukiwa huyo ilizorota kwa haraka na inakisiwa aliaga dunia kutokana na maradhi ya saratani ya ini.
Bwana al-Liby alikamatwa na vikosi maalum vya marekani nchini libya mwaka 2013.
Alilalamika kuwa alikuwa ametekwa na kudhalilishwa
Amekana kuhusika kwenye mashambulizi ya Nairobi na Dar-es- salam ambapo zaid ya watu 220,000 waliuawa.