Magari ya Tanzania Jomo Kenyatta


Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta
Serikali ya Tanzania imesema itawasiliana na Serikali ya Kenya ili kulipatia ufumbuzi tatizo la magari ya wafanyabiashara wa Tanzania ambayo yamezuiwa kuingia kwenye Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya kupeleka na kuchukua wageni.
Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania ambao wanafanya biashara hiyo wamesema magari yao yalizuiwa na maafisa wa Kenya tangu Desemba 22 mwaka kwa madai kwamba ni amri kutoka ngazo za juu za utawala wa Serikali ya Kenya.
Akiongea na BBC kwa njia ya simu kutoka Arusha kaskazini mwa Tanzania mmoja ya watanzania anayemiliki wa magari yanayofanya biashara ya kubeba na kupeleka wageni katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya Moses King'ori siku ya zuio hilo magari yao yalipofika katika lango la Uwanja wa ndege yaliambiwa hayaruhusiwi kuingia.
Kufuatia zuio hilo la magari ya wafanyabiashara wa Tanzania, serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu aliongea na BBC kwa njia ya simu kutoka Singida katikati mwa Tanzania amesema inawasiliana na serikali ya Kenya ili kulipatia ufumbuzi sakata hilo.
Kufuatia zuio baadhi ya wanyabiahsha wanafanya biashara hiyo wamesema wameanza kuathirika kwani inawalazimu kuwashusha wageni na kutafuta usafiri mwingine kwenda na kutoka katika uwanja huo wa ndege
Zuio hili la wafanyabiashara wa magari kutoka Tanzania wanaobeba na kupeleka wageni kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa kiasi fulani huenda likatikisa uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia wa nchi hizo marafiki kama halitapatiwa ufumbuzi wa haraka.