Hivi ndivyo Mgomo wa Daladala jana Jijini Mwanza


Daladala zikiwa zimepaki katika Jiji la Mwanza kutokana na mgomo wa madereva.
Taswira kutoka maeneo ya Jiji la Mwanza baada ya mgomo wa waendesha daladala.
Na  Waandish Wetu, Mwanza
WAENDESHA magari ya kusafirisha abiria katika ya Jiji la Mwanza maarufu kama daladala leo wamefanya mgomo na kuziba njia zote zinazoingia mjini kutokana na maeneo waliyokuwa wanaegesha magari yao kwa ajili ya kusubiri abiria (stendi) kugawiwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga kwa aijili ya shuhuli zao.
Daladala zikiwa zimeegeshwa wakati wa mgomo.
Hali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Stendi ya Tanganyika na Stend ya Soko Kuu jijini Mwanza ambapo yanaegesha magari ya kwenda Airport, Ilemela, Bwiru na Mwaloni ambapo madereva hao waliziba njia zote zinazo ingia kwenye maeneo hayo.
Mwenyekiti wa waendesha daladala Mkoani Mwanza, Hassan Dede Petro alisema hali hiyo imejitokeza kutokana na wafanyabiashara hao kuanza kugawana maeneo kwenye stendi hizo bila uongozi wa waendesha daladala kuwa na taarifa yeyote kuhusu suala hilo.
''Hali hii imejitokeza kwa sababu ya wafanyabiashara wadogodogo kuanza kujigawia maeneo katika eneo letu ambalo tunaegesha kwa ajili ya kusubiri wateja wetu (abiria)'' Alisema Petro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo 'machinga' Said Tembo alisema walichukua uamuzi huo kutokana na kupata ruhusa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Magesa Mulongo kuwa watumie maeneo hayo kwa shuhuli zao za kufanyabiashara kwenye maeneo ya stendi hizo.
(PICHA NA WAANDISHI WETU JIJINI MWANZA)