Dc Kilasi: Viongozi wa Saccoss angalieni michanganuo


VIONGOZI wa saccos hapa nchini wametakiwa kutazama kwa umakini michanganuo ya wanachama wao wanao hitaji mikopo ili kukabiliana na tatizo la kuwapo kwa watu wanao shindwa kulipa malejesho ya mikopo yao.

Hayo yamebainishw ana mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe wakati wa uzinduzi wa Saccos ya Vijana Ulembwe Saccos limited ya wilayani humo, amesema kuwa uongozi wa saccos uangalie kwa makini mchanganuo kwa lengo la kukupisha mtu anayeweza kurejesha mkopo.

Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya kuto rejeshwa kwa mikopo katika saccos nyingi hapa nchini kutokana na wakopaji kuto kuwa na michanganuo sahihi wa pesa anayokopa.


Amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa wakijiingiza katika mikopo kwa kuiga na kujikuta wakibadilisha sehemu za kukopa kwa kulipa madeni katika saccos za awali.


Kwa upande wake wananchi na viongozi wa Kijiji Cha Ulembwe ambapo nio makao makuu ya sakosi hiyo wamewataka vijana kujiunga katika vikundi mbalimbali zikiwemo sakosi ili kuweza kusaidiwa na serikali katika mikopo yake kwa vijana.

Katibu wa saccos amesema kuwa kupitia hapo wataweza kuwakopisha vijana hasa zile pesa za serikali zilizo tengwa kwajili ya vijana na wanawake kwa kuwa hapo ni sehemu ambayo ni salama na inaaminika kama anavyo eleza.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Ulembwe, Peter Luhasi amewataka wananchi hao waliojiunga katika sakosi hiyo na kupata mkopo wa pembejeo za wakati wa uzinduzi wakawe mabarozi wazuri kwa wenzao ili nao wajiunge, huku diwani wa kata hiyo akipongeza juhudi za wananchi waliojiunga ma saccos hiyo na kunufaika na matunda ya mikopo.


Aidha mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Yohanes Chongolo amehimiza wananchi kujitokeza kujionga ili kuunganisha nguvu katika sakosi kwa kuwa kwa mwananchi wa sasa bila kupopa hawezi kufanya maendeleo sabidi lakiji wakiunganisha mitaji yao wataendelea kwa kukopeshana.