TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KUTOKA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YATEMBELEA MELI YA KIHISTORIA YA MV LIEMBA


Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata fursa adhimu ya kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba iliyo kwenye Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.

Wakizungumza mara walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha bashasha waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe iliyo na umri zaidi ya miaka 100.

Mmoja wa wakaguzi hao Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana kuingia na kushuhudia mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini Tanzania.

“Nimefurahi sana kufika leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya ukongwe wake bado inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka mingi zaidi,” alisema.

MV Liemba ni meli ya Kitanzania inayohudumia pwani za Ziwa Tanganyika. Ni chombo cha usafiri wa majini chenye umri mkubwa kuliko kingine chochote nchini na kipo tangu mwaka 1914. Meli hii kama zilivyo meli ningine inasukumwa na injini ya diseli na ina urefu wake ni mita 67, upana mita 10 na uzito wa tani 1500.

Kwa mujibu wa Nahodha wa meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi, meli hiyo ina uwezzo wa kubeba abiria 600 na tani za mizigo 200.

“Katika daraja la kwanza meli ina uwezo wa kubeba abiria 20, daraja la pili abiria 30 na daraja la tatu abiria 550,” alisema. 

Meli ya MV. Liemba inamilikiwa na Kampuni ya MSCL na kusajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa namba ya usajili KP/P001. Meli hiyo ilijengwa katika Bandari ya Kigoma mwaka 1913 na mjenzi kutoka Ujerumani kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo na abiria.

Mv. Liemba ilitengenezwa nchini Ujerumani mwaka 1913 ikiwa ikiitwa kwa Kijerumani "Graf von Goetzen" kwenye kiwanda cha meli cha Meyer huko Papenburg.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe duniani.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni ndani ya MV Liemba. Kulia ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi.
Nahodha wa MV Liemba, Kapteni Mathew Mwanjisi (Watatu kushoto) akitoa maelezo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kulia) akiiongoza Timu yake kusikiliza kwa umakini namna ya kusoma radar inayotumika ndani ya Meli ya MV Liemba. Anayewapa maelezo ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi.
Nahodha wa Meli ya MV Liemba, Kapteni Mathew Mwanjisi (Kulia) akitoa maelezo ya namna ya kutumia chombo cha kuokolea kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wanaomsikiliza ni Kiongozi wa Timu hiyo, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Abdallah.
Mhandisi Mkuu wa Meli ya MV Liemba, Eng. Justine Joachim (Mwenye fulana nyeusi) akiwapa maelezo Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipongia kujionea mitambo ya kuendeshea meli hiyo.
Kazi inaendelea! Watumishi wa Meli ya MV Liemba wakiendelea na kazi ya kushusha shehena ya mahindi kutoka kwenye meli hiyo. PICHA NA SAIDI MKABAKULI

WENYEVITI WA TAIFA WA VYAMA VYA NCCR -MAGEUZI ,JAMES MBATIA NA TLP,AGUSTINE MREMA WAWANADI WAGOMBEA WAO JIMBONI VUNJO.

Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi akiendelea na mikutano ya kampeni katika kijiji cha Kisangesangeni kata ya Kahe akiwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti.
Msafara wa Pikipiki ukiongoza kuelekea kijiji cha Ngaseni kwa ajili ya mikutano ya kampeni ya chama cha NCCR-Mageuzi.
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika kijiji cha Ngaseni B,Amfrosia Komba akizungumza wakati akiomba kura kwa wananchi wa kijiji hicho.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi taifa ,James Mbatia akimnadi mgombea uenyekiti wa kijiji cha Ngaseni B,Amfrosia Komba ambaye alijitambulisha kuwa binti wa mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi ,Kepteni John Komba.
Wanakijiji wa Ngaseni B,wakifuatilia mkutano.
Wagombea wa nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri ya kijiji cha Ngaseni wakitoa salamu za chama cha NCCR-Mageuzi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho.
Wanakijiji wa kijiji cha Ngaseni B,wakiitikia salamu ya chama cha NCCR-Mageuzi.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akigawa vitabu kwa wakazi wa kijiji cha Ngaseni.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akiwasili katika kijiji cha Kahe ,jimbo  la Vunjo kwa ajili ya mkutano wa kampeni wa kuwanadi wagombea wa nafasi za uenyekiti.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akiwatuza vijana waliojitokeza kutoa burudani katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Kahe.
Wananchi katika kijiji cha Kahe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa kuwanadi wagombea wa nafasi za uenyekiti katika kijiji cha Kahe. 
Mwenyekiti Mbatia akiwahutubia wanakijiji wa Kijiji cha Kahe katika mkutano wa kampeni wa kuwanadi wagombea katika vijiji mbalimbali katika jimbo la Vunjo.
Mwenyekiti Mbatia akiwahutubia wanachi katika kijiji cha Orio jimboni Vunjo..
Mwenyekiti Mbatia akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Uchira jimboni Vunjo.
Wakati Mbatia akiendelea na mikutano katika mikutano yake ,Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Agustine Mrema naye amefanya mikutano yake katika vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji cha Mamba Kotela kama anavyoonekana katika picha.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii kanda ya kaskazini.