Polisi afa ajalini Njombe

WATU wamefariki dunia mkoani Njombe katika matukio tofauti ya ajali za barabarani likiwemo la askali polisi kupinduka na gari na kusababisha kifo chake hapo hapo katika maeneo ya Tanwat  barabara ya Igawilo – Lupembe  mkoani hapa baada ya gali yake kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe FulgenceNgonyani alisema kuwa katika tukio la kwanza lilitokea Disemba 20 majira ya saa 5:45 usiku, Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha Makambako alipata ajali akiwa na gari ya polisi yenye namba PT 0766 katika maeneo ya Igawilo kata ya Ikuna Wilayani Njombe.

Ngonyani alimtaja askari huyo aliye fariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni mwenye namba F 6435 PC Mahamoud Ndauka (32) ambapo katika ajali hiyo gali aliyo kuwa nayo aina ya Land Rover pick up nail ya jeshi hilo katika wilaya ya kipolisi Makambako, lilipinduka baada ya kuacha njia.

Alisema kuwa askali huyo alikuwa ni dereva wa police na alikuwa mkazi wa line polisi Makambako na kuwa chanzo cha ajali hiyo kinaendelea kuchunguzwa kwani bado hakijajilikana.

Aidha Ngonyani alisema kuwa katika tukio la pili ambalo lilitokea majira ya saa 3:45 usiku katika maeneo ya Mizani Makambako barabara ya Makambako – Iringa mwanaume asiye fahamika jina aligongwa na gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili IT 9311.

Alisema kuwa dereva aliyekuwa akiiendesha gali hiyo Anord Mwanyanje mkazi wa Jijini Dar es Salaam (35) anashikiliwa na jeshi hilo na atafikisha mahakamani upelelezi utakapo kamilika.

Alisema kuwa gari hiyo ni mali ya Julieth Kweyambe inashikiliwa na jeshihilo katika kituo polisi Makambako.

Aliongeza kuwa jeshi hili linaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kitamfikisha dereva huyo mahakamani baada ya kubaini chanzo cha ajali hiyo.