Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya ATC wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari zao kuarishwa. Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka liniZenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.
Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro….Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.