WATENDAJI wa vijiji wametakiwa kufichua wanao tumia vibaya
vyandarua vinavyo gawiwa na serikali kwa wananchi ili kutimiza lengo la
kufikisha asilimia 85 ya umiliki wa vyandarua ifikapo mwaka 2015.
Akizungumza katika kikao cha uhamasishaji kugawa vyandarua
vya gralama nafuu kwa viongozi wa mkoa na wajumbe wa uendeshaji wa huduma ya
afya mkoa wa Njombe, Mganga mkuu wa Mkoa Dr Samuel Mgema alisema kuwa watendaji
wa vijiji wanatakiwa kuhusishwa sana katika zoezi hili.
Alisema kuwa viongozi hao kwa kuwa ndio wapo karibu sana na
wananchi wataweza kuwafichu wanao tumia vyandarua vibaya na kuwawajibisha.
“Viongozi wa vijiji wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha zioezi hili linaenda kama ilivyo takiwa na kuhakikisha wananchi wanatumia katika matumizi sahihi kulingana serikali ilivyo kusudia, kuwani kuna wananchi wamekuwa wakitumia vyandarua hivyo kwa kufugia kuku na wao wakilala bila chandarua,” Alisema Dr Mgema.
Alisema kwa kufanya hivyo serikali itatimiza malengo yake ya
kubaki na kazi ya kuhakikisha wananchi wanatumia vyandalua hivyo ambavyo
wamegawiwa.
Kwa upande wake mgeni rasm, Katibu tawara msaidizi mkoa wa
Njombe, Gideon Mhami alisema kuwa kwa mkoa wa Njombe kuwamekuwa na asilimia 11
ya wahonjwa ma maralia kiasi mbacho inatakiwa kupungua.
Alisema kuwa kufuatia kampeni hii ambayo itazinduliwa hivi
karibuni na Rais Dkt. Jakaya Kikwete oktoba 10 hadi 24 mkoani Dodoma wananchi wanatakiwa
kupata elimu ya kutosha ili kuwafikia bila kikwazo.
Wananchi kama watapatiwa elimu juu ya utolewaji wa vyandarua
hivyo watajitokeza na kuchukua kwaajili ya kujikinga na maralia ambayo yanaua
watoto na mama wajawazito kwa wingi.
Naye muwezeshaji kutoka wizara ya Afya na Ustawi wajamii
kitengo cha maralia Mwafongo John alisema kuwa serikali itasambaza vyangarua
hivyo vya bei nafuu moja kwa moja kwa wananchi kwa mikoa 22 isipo kuwa mikoa
mitatu ya kusini.
Alisema kuwa mikoa ambayo haita husishwa na mpango huu ni
pamoja na Ruvuma, Lindi na Mtwala kwa mikoa hiyo ipo katika mpango mwingine wa
ugawaji wa vyandarua mashuleni.
Hivyo alisema kuwa vyandarua hivi katika mikoa hiyo itakayo
gawiwa ni kwa lengi la kufiakia asilimia 85 ya umiliki wa vyandarua kwa
watanzania wote na kubaki na mkakati wa kuhakikisha vinatumiwa kwa usahihi.
Alisema matumizi ya vyandarua hapa nchini kuna baadhi ya
mikoa ambayo hali ya hewa inafanana hata matumizi yake yanafanana, na kutolea
mfano wa mkoa wa Njombe matumizi yanafanana na Arusha kwa sababu wakazi wake
wanaona mbu hakuna na kuacha matumizi ya vyandarua.
