
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Kilolo
Profesa Peter Msola, alipowasili eneo la Kilolo Minadani, na kufanyiwa
mapokezi, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani
ya CCM, katika jimbo hilo, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo, Oktoba
8, 2014. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Seti Mwamoto

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na mwenyeji wake, Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Kilolo, Seth Mwamoto baada ya kuwasili katika jimbo la
Kilolo wilayani humo leo,
Vijana
waliojiajiri katika kikundi cha Muungano cha ufyatuaji matofali katika
jimbo la Kilolo, wilayani Kilolo mkoani Iringa wakiwa kazini
alipowatembelea Kinana leo, Oktoba 8, 2014. Zaidi ya vijana 40 wamo
katika muungano huo.
+akifuatilia+matukio+ziara+ya+kinana+Kilolo.jpg)
Mjumbe
wa Kamati ya Utekelezaji, Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Seki Kasuga
(kushoto) akifuatilia matukio Kinana alipotembelea Umoja wa
wajasiariamali wa kikundi cha kufyatua matofali kwa teknolojia ya kisasa
katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo mkoani Iringa leo

Kinana
akizungumza na vijana hao kabla ya kushiriki ufyatuaji matofali. Kulia
ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye anayefuatana na Kinana
kwenye ziara hiyo ya mkoa wa Iringa

Kinana
akisisitiza jambo alipozungumza na vijana wa kikundi hicho kabla ya
kushiriki ufyatuaji matofali. Kinana alizitaka mamlaka zinazohusika
kuwapatia vijana hao eneo lenye maji ya uhakika kwa ajili ya ufyatuaji
matofali, baada ya kumweleza kuwa pamoja na kuufurahia mradi huo wa
ufyatuaji matofali lakini wanakumbana na changamoto ya kukosa maji kwa
kuwa eneo wanalofanyia mradi huo halina maji.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali akiwa na
Prof. Peter Msola (kushoto), alipotembelea mradi wa vijana wajasiriamali
wa kikundi cha ufyatuaji matufali kwa teknolojia ya kisasa katika jimbo
la Kilolo wilayani Kilolo mkoani Iringa, leo

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua alipotembelea mradi
wa vijana wajasiriamali wa kikundi cha ufyatuaji matufali kwa
teknolojia ya kisasa katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo mkoani
Iringa, leo

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofal,
alipotembelea mradi wa vijana wajasiriamali wa kikundi cha ufyatuaji
matufali kwa teknolojia ya kisasa katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo
mkoani Iringa, leo

Katibu Mkuu wa CCM akipanga matofali baada ya kushiriki ufyatuaji wa matoli kwenye mradi huo wa vijana wa Kilolo

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi kwenye Halmashauri
ya Kilolo, pamoja naye Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita
BAADAYE KINANA ALIENDA KUCHAPA KAZI IHIMBO

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye viwanja vya
zahanati ya Kijiji cha Utengule kata ya Ihimbo, kabla ya kukagua ujenzi
wa zahanati hiyo, kwenye jimbo la Kilolo, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
leo

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye viwanja vya zahanati hiyo ya Kijiji cha Utengule

Wananchi
wakisoma utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyofanywa na Mbunge wa Kilolo
Profesa Peter Msolwa, Kinana alipowasili kwenye zahanati hiyo

Mbunge wa Kilolo Profesa Msola akieleza alivyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo kwenye mkutano huo
,+Parcras++Mkakatu+akisikiliza+maelekezo+ya+Kinana+wakati+wa+mkutano+kwenye+zahanati+ya+Kijiji+hicho.jpg)
Mwenyekiti
wa serikali ya Kijiji cha Utengule kwa tiketi ya Chadema, Parcras
Mkakatu akisikiliza maelekezo ya Kinana wakati wa mkutano kwenye
zahanati ya Kijiji hicho
Mwenyekiti
wa serikali ya Kijiji cha Utengule (Chadema), Parcras Mkakatu
akijieleza kwa Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
Mwenyekiti
wa serikali ya Kijiji cha Utengule (Chadema), Parcras Mkakatu
akijieleza kwa Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho

Wazee
wa Kihehe wakimpamba Kinana kwa mavazi rasmi ya keshima ya kabila hilo
katika kijiji cha Utengule, baada ya kuhutubia wananchi kwenyeviwanja
vya zahanati ya Kijiji hicho

Kisha wazee hao wakampa mkuki kukamilisha heshima hiyo

Kinana akishuka jukwaani baada ya kuwashukuru wananchi kwa wazee hao kumpa heshima ya uchifu

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi wa Kiijiji cha
Utengule baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Zahanati ya Kijiji hicho leo,Oktoba 8, 2014. Picha zote na Bashir
Nkoromo-theNkoromo Blog