Afisa wa ngazi ya
juu kwenye mji wa mpaka wa Kobane nchini Syria amiambia BBC kuwa
wanamgambo wa Islamic State wamejaribu kukishambulia kivuko cha mpaka na
Uturuki lakini wakashindwa kukidhibiti kivuko hicho.
Khalid
Berkel amesema kuwa wanamgambo hao wameshambulia mji wa kobane kutoka
pande tofauti katika jitihada za kuuzingira kabisa ambapo wamepiga hatua
kutoka maeneo ya mashariki kwa kutumia mabomu yaliyotolewa kwenye
magari.Wapigani wa kikurdi na wanajeshi huru nchini Syria wanasema kuwa wanahitaji kwa dharura silaha nzito.
Maelfu ya raia wamekwama kwenye miji wa kobane na umoja wa mataifa umeonya kuwa kutatokea mauaji ya halaiki iwapo mji huo utatekwa .
Awali wito ulitolewa nchini Syria na Iraq wa hatua za dharura kuchukuliwa dhidi ya wanamgambo hao
Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa nchini Iraq kwenye mji ulio magharibi mwa Anbar wameitaka serikali yao kuomba msaada wa vikosi vya nchi kavu vya Marekani katika vita dhid ya ISIS.
