MSANII HUYO AMEPANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA.
Msanii wa Hip Hop, Rashid
Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia
katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es
Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam. (Picha
na Francis Dande)
Msanii wa Hip Hop, Rshid
Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa
askari Polisi.
Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi
Benzi’
akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu
likiwemo la
kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Msanii
wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro
‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la
matumizi ya dawa za kulevya.
Chid
Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu
Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo
atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata
kei’ ili avae vizuri
nguo.
Akisomewa
mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai
kwamba mnamo
24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege
wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alidai
kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa
na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia
shitaka la
pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye
thamani 1,720.
Mbali
na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa
vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha
nazi
kitupu na kijiko kimoja.
Hata
hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri
hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba
11,
mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.
Hakimu
Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa
na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.
Hali
hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya
simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini
wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.
Chidi
Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya
ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya,
juzi jioni
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam