Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bw. Titus Mkapa akimkaribisha Mwenyekiti wa timu ya
Wizara HUM Sports Club (hayupo pichani) ili atoa salama za wachezaji
kwa mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo
leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (HUM Sports
Club) Dkt. Margareth Mtaki akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga
wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani
Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa
Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga
wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani
Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akimkabidhi zawadi Mwanamichezo aliyeiletea Wizara ushindi katika
mashindano ya SHIMIWI na Meimosi mwaka jana Bibi. Niuka Chande.
Mchezaji huyo aliibuka mshindi katika michezo ya Draft na kurusha Tufe
na kuiletea Wizara vikombe viwili. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara
Dkt. Margareth Mtaki.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo jijini Dar es Salaam wakati
wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara hiyo wanatarajia kwenda
mjini Morogoro kesho kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza
kuanzia tarehe 27 septemba hadi Oktoba 11.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akiwa amenyanyua juu Kikombe cha ushindi wa kwanza kwa mchezo
wa Draft katika mashindano ya SHIMIWI mwaka jana ambacho kilinyakuliwa
na mchezaji watimu ya Wizara ya Habari Bibi. Niuka Chande (mwenye taki
suti nyeusi)kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante
Ole Gabriel akifurahia
Baadhi
ya wachezaji wa timu ya HUM Sports Club wakitoa salaam za timu yao kwa
mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya
kuwaaga wachezaji wa timu hiyo wanakwenda mjini Morogoro kushiriki
mashindano ya SHIMIWI yanayotarajiw kuanza tarehe 27 mwezi huu na
kumalizika tarehe 11 Oktoba.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na
wachezaji wa timu ya Wizara itakayoshiriki mashindano ya SHIMIWI mwaka
huu.Waliokaa kutoa kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa TBC Joyceline Lugora,
Mwakilishi wa Kampuni ya Water.Com(T) Ltd Juma Rajab Mboge, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya HUM Sports Club Dkt. Margareth
Mtaki.
Picha zote na Frank Shija, WHVUM.