SHUHUDA ALBINO ATAKA WAUAJI WANYONGWE HADHARANI


DSC_0519
Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

=======  =======  =======
Mwanamke albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.

Alisema hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi. Akiongea kwa uchungu huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi cha kushidwa kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono yake alikuwa na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili hao si wa kusamehewa.

Alisema akiwa mama wa familia kitendo cha kumuondolea mikono yake kimemfanya kuwa tegemezi hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu ambayo anayo ya kunyanyapaliwa na jamii.

Alisema hayo wakati akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Alisema japokuwa Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye ulemavu wa albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi. Alisema kwa sasa Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo sasa linajificha na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
DSC_0534
Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.

Alisema ni vyema jamii ikawatazama na kuwasaidia kwa kuhakikisha kwamba wanasaidia kuwafichua watenda maovu hao hasa ikizingatiwa kwamba watu wenye albinizimu ni watu na watu kama watu wengine na hawawezi kuwa chanzo cha utajiri kwa binadamu wenzao.
Alisema anatamani kuona waliotiwa hatiani wakiuuawa hadharani au hata watu hao nao kukatwa viungo vyao ili watambue jinsi isivyofaa kuwafanyia binadamu wenzao matendo hayo.
Alishukuru taasisi ya Under the Same Sun kwa kumsaidia toka aliponyofolewa mikono mpaka leo na kuhimiza serikali kuona namna ya kuwasaidia waliokatwa viungo vyao ili waweze kusihi maisha ya kawaida.
DSC_05401
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja hivi karibuni jijini Dar.
Pamoja na kuomba watu hao wanyongwe Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju aliitaka jamii kutambua kwamba sheria ya kuua anayeua ipo lakini inakabiliwa na mashindano na wanaharakati huku watoa ushahidi wakishindwa kuisaidia mahakama kufikia maamuzi katika kesi za maalbino.
Alisema ni wajibu wa wananchi kusimamia amani kwa kuhakikisha wanaisaidia serikali kutekeleza wajibu wake.
DSC_0384
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
Naye Balozi wa Uturuki nchini alisema kwamba Ali Davutoglu amesema kwamba ujenzi wa kituo cha maalbino Bagamoyo utaanza hivi karibuni ili kuwapatia nafasi wananchi hao kuwa katika hali ya kawaida.
Kituo hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchukua watu 500 na kuwa chemchem ya maarifa kwa watu wenye albinizimu.
Katika adhimisho hilo watoto wenye albuinizim walitoa shoo ya nguvu iliyowafanya watu mbalimbali kujimwayamwaya katika eneo la wazi na kutoa zawadi kwa vijana hao.
Aidha bendi ya vijana ilitumbuiza na kwaya ilikuwepo kutoa ushaiwishi wa kuelewa umuhimu wa amani huku wazungumzaji wengine wakitaka wanasiasa kuhudhura maadhimisho hayo na kupeleka ujumbe kwa wananchi ambao wanawasikiliza.
Katika adhimisho hilo wanasiasa waliokuwepo ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa dar es salaam, Madabida, Kaimu katibu Mkuu NCCR-Mageuzi Faustin Sungura na Naibu katibu mkuu CUF Magdalena Hamis Sakaya ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu Tabora.
DSC_0575
Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju, akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar.
DSC_00521
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa  Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid (wa pili kushoto), Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi, kwenye picha ya pamoja na binti mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (kushoto).