Makubaliano ya ujenzi mpya wa Gaza yafikiwa

Makubaliano ya unjenzi mpya wa Ukanda wa Gaza kati ya Israel na Hamas yamefikiwa kutokana na juhidi za Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inatoa jukumu kubwa la uongozi kwa mamlaka ya Palestina huku ikihusishwa sekta binafsi

Palästinenser Unterkünfte nach der Offensive 17.09.2014 Gaza Eneo la Ukanda wa Gaza
Afisa wa Umoja wa mataifa Robert Serry amesema makubaliano kati ya Israel, Mamlaka ya Palestina na Umoja wa Mataifa yanajumuisha waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao jukumu lao kubwa litakuwa kuhakikisha vifaa vya ujenzi au malighafi za ujenzi havitaondoshwa katika mikono ya raia na kuingizwa katika matimizi ya kijeshi.
Kwa mujibu wa Palestina na maafisa wa Umoja wa Mataifa vita vya kikali vya Gaza, vimesababisha zaidi ya Wapalestina 2,100 kupoteza maisha, wengi miongoni mwa hao wakiwa raia wa kawaida. Israel inasema idadi ya wanamgambo walikufa ni zaidi ya inayotajwa na Palestina na kulituhumu kundi la wapiganaji la wanamgambo wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao yake. Upande huo wa Israel unasema wanajeshi wake 66 wameuwawa na raia sita.
Hali mbaya Ukanda wa Gaza
Gaza hofft auf Wiederaufbau Mwaathirika wa mapigano ya Hamas na Israel mjini Gaza
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, Robert Serry amesema katika ziara yake mjini Gaza wiki iliyopita alishuhidia kiwango cha kushtusha cha uharibifu wa miuondombinu, hospitali na mashule.
Eneo kubwa la Ukanda huo limeharibiwa vibaya na inakadiriwa takribani nyumba 18,000 zimebomolewa kabisa. Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kiasi ya watu 100,000 wameachwa bila ya makazi. Zaidi ya watu 65,000 mpaka hivi sasa wanaishi wanahifidhiwa kwa muda katika eneo la Umoja wa Mataifa.
Mgogoro wa Kibinaadamu
Aidha kiongozi huyo wa Ujumbe wa Umoja Mataifa katika eneo hilo aliongeza kusema mgogoro wa Gaza ni janga la kibinaadamu na kusabisha gharama kubwa. Na kutaka baraza la usalama kuunga mkono ili kujenga hali ya kujiamini kwa mataifa wahisani."
Wakati makubaliana ya kuweka silaha chini yaliyosimamiwa na Misri agost 16 kwa kiasi kikubwa yanatakelezwa lakini bado hali imaeendelea kuwa tete na hasa katika kushughulikia masuala ya msingi ambayo bado hayajatekelezwa.
Wiki iliyopita makamu wa waziri mkuu wa Palestina, Mohammed Mustafa alisema mataifa wafadhili wanasita kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Gaza kwa sababu kundi la Hamas bado limeendelea na udhibiti wa eneo hilo na kunaonekana uwezekano wa kuendelea kwa vita. Mustafa ambae ni afisa wa ngazi ya juu wa Mamlaka ya Palestina alisema vyombo vya kimataifa vina hamasa kubwa kuona jeshi la rais Mahmoud Abbas linashika hatamu ya usimamizi katika eneo la Gaza.
Mwandishi: Sudi Mnette APE