Hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa rais wa Misri,
Hosni Mubarak, imeahirishwa kwa mara nyengine tena, kufuatia jaji
aliyekuwa anaiongoza, Mahmoud al-Rashedi, kusema hatua hiyo
itaipa mahakama nafasi zaidi ya kuitathmini kesi hiyo. Hosni
Mubarakak anadaiwa kupanga mauaji ya waandamanaji wakati wa
maandamano ya kutaka mabadiliko yaliotokea mwaka 2011. Polisi
nchini humo imesema, Mubarak aliye na miaka 86 alisafirshwa kwa
helikopta katika mahakama hiyo iliyoko katika chuo cha kijeshi nje ya
mji wa Cairo. Rais huyo wa zamani wa Misri, aliyeiongoza nchi hiyo
kwa miongo mitatau ameshtakiwa pamoja na makamanda wake saba
wa usalama kwa kuhusika na mauaji ya mamia ya waandamanaji
wakati wa siku 18 za maandamano ambayo hatimaye yalimng'oa
madarakani. Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 29 mwezi wa
Novemba mwaka huu.