Baadhi
ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la
Fiesta 2014 lenye kauli mbiu (sambaza upendo) wakiwasili mapema leo
mchana nyumbani kwa Mama Mkwe wa Afande Sele,mtaa wa Amani mjini
Morogoro kwa madhumuni ya kutoa pole kwa Afande Sele pamoja na Familia
ya marehemu ya aliyekuwa Mzazi mwenzake Afande Sele,Marehemu Asha
aliyetambulika zaidi kwa jina la Mama Tunda,ambaye leo anatimiza siku
Arobaini tangu afariki na kuzikwa.
Baadhi
ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo katika tamasha la
Fiesta pichani wakiwa katika suala zima la kufariji wakiwemo Wazee wa
eneo hilo ambao walifika kwenye shughuli ya kutimiza siku Arobaini tangu
kufariki kwa mke wa Afande Sele aliyekuwa akiishi nae kwa takribani
miaka 17 na kufanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Tunda na Asante
sanaa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mo Music anaetamba na wimbo wake wa Basi nenda unaofanya
vyema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini,akitoa mkono wa
pole kwa Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii
Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akitoa mkono wa pole kwa
familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii
Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi,Joe Makini
akitoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda
(aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini
Morogoro mapema leo mchana.
Mtoto
wa kwanza wa Afande Sele,aitwaye Tunda akisalimiana na baadhi ya
wasanii waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa
marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi
kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo
mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu
kufariki kwake.
Afande
Sele akiwa na watoto wake wawili alioachiwa na Marehemu Mama
Tunda,ambao ni Tunda na Asante Sanaa wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya
Globu ya jamii mapema leo mchana.
Afande Sele akiwa na watoto wake wawili alioachiwa na Marehemu Mama
Tunda,ambao ni Tunda na Asante Sanaa wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya
Globu ya jamii mapema leo mchana.
Baadhi
ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la
Fiesta 2014,ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakiwa na baadhi ya ndugu jamaa
na marafiki wa Familia ya marehemu Mama tunda,ambapo leo inafanyika
arobaini yake,mtaa wa Amani mjini Morogoro.
Baadhi ya wasanii wakiwa wametulia wakitafakari yao.
Pichani kulinia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Leo Tena kutoka Clouds FM,Da Husna akiwa na mtoto wa Afande Sele,aitwaye Tunda.
Msanii
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Mkali wa Rhymes Afande Sele
akiushukuru Uongozi wa Clouds Media Group sambamba na kuwashukuru
Wasanii hao waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa
marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi
kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo
mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu
kufariki kwake.
Afande
Sele akizungumza kwa kuwataka wasanii kuungana na kuwa kitu kimoja
katika shida na raha,kuacha tabia ya kubaguana na kujengeana chuki
ambako kumekuwa ni sehemu ya kuufanya muziki wao na mambo yao mengi
yasifanikiwe ipasavyo,Hivyo amewashauri wasanii kuwa na roho ya
kupendana na kufanya kazi zao kwa kujituma na ubunifu ili tasnia ya
muziki iweze kufika mbali zaidi.
Ommy Dimpoz katika picha ya pamoja
Da Husna wa Leo Tena ya Clouds FM katika picha ya pamoja
Afande Sele akishoo love na Ommy Dimpoz.