Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia vijiji kadha na makanisa kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wakaazi wa huko walisema kuwa watu wengi wameuwawa na nyumba nyingi zimeteketezwa.Mashambulio yamefanywa karibu na mji wa Chibok, ambako wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa nyara mwezi wa Aprili.
Mwandishi wa BBC Nigeria anasema katika kijiji kimoja cha Kautikari, wanamgambo wa kijiji walizidiwa nguvu walipojaribu kulinda kanisa.
Anasema jeshi halikuweza kufika katika vijiji hivyo vilioko mbali.