WALIMU wanaotaka kuanzisha chama chao tofauti na chama cha
walimu Tanzania (CWT) watakiwa kutokianzisha chama hicho, badala yake wapendekeza
mapungufu ambayo yanayohitajika kuondolewa katika chama cha walimu ili kuto
tokea mgawanyiko.
Akizungumza na viongozi wa wanawake wa chama cha walimu
Tanzania mkoa wa Dodoma (CWT) aliyekuwa waziri wa elimu mbunge wa viti maalum
Margret Sitta (CCM) jana alisema kuwa walimu wanatakiwa kuboresha chama ili
kiwe na nguvu ya kudai haki zao na siyo
kuwa na mitazamo ya kuanzisha chama kingine.
Mbunge huyo alisikitishwa na baadhi ya kauli za walimu
ambao wanaotaka kuanzishwa kwa chama kingine, alisema kitendo hicho ni uchu wa
madaraka wa kutokana na kukiacha chama chao cha CWT ambacho kwa sasa kinaendelea kutetea wanataaluma
ya ualimu.
Sitta alisema kuwa kuanzishwa kwa chama kingine cha waalimu
hapa nchini kutapunguza nguvu waliyo nayo kutoka na na chama hicho.
“Nilisikitishwa siku moja tuko bungeni walikuja watu wanao
taka kuanzisha chama kingine cha waalimu, hivi tutakuwa waalimu mtakuwa na
mgawanyiko sana na mtashindwa kuwa na umoja ambao mnao hivi sasa kwa kuwa kila
chama kitakuwa na madai yake,” alisema Sitta.
Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa chama kingine cha waalimu
waalimu wa takuwa wameanza kugawanyika kwa sabau kila chama kitakuw ana madai
yake kutoka na chama kinavyo jisikia tofauti na sasa kumekuwa na sauti moja ya
waalimu.
Alisema wanaotaka kuanzisha chama kingine wanatakiwa kuwa karibu na chama ili kujua nini chama hicho kina mapungufu
gani ili kufanya marekebisho na kukiwezesha kuwa na maendeleo kwa ajili ya
walimu.
Aliongeza kuwa mgawanyiko hautawanufaisha bali utazorotesha katika
kudai mahitaji yenu kutokana na jitihada
zilizopo za ambazo zimefanya chma kupata
mafanikio ya kuwasaidia waalimu wengi
kutatua shida zao na kujenga majengo yao
kila mkoa hapa nchini kutoka na pesa zinazo changwa na wanachama kila mwezi.
Alisema chama kwa sasa kinaweza kufanya maamuzi yake kutoka
na kuwa na vitega uchumi vyake na kutatua kwa urahisi matatizo wanayo kabiliana
nayo waalimu kote nchini.
