
Mwili
wa mtu aliyeuawa kikatili kwa kukatwa kichwa ukiwa katika gari la
polisi baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga
jana asubuhi kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio mtu huyo
alifanyiwa unyama huo nyakati za usiku wa kuamkia leo ambapo mwili wa
mtu huyo ulitupwa kando ya daraja la mto katusa ambako pembeni yake kuna
makaburi katika mtaa wa Tambazi katika Manispaa ya Sumbawanga.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tambazi, Christopher Kwimba alisema kuwa mtu huyo
aliyeuawa anakadiriwa kuwa na umri katika ya miaka 25 na 27 hivyo ni
vigumu kumtambua kwa haraka kutokana na wauaji kuondoka na kichwa chake.

Baadhi
ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa kwa kukatwa
kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia leo kwa ajili
ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya
mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.HABARI NA PICHA KWA HISANI YA BLOGU YA
PEMBEZONI KABISA