Makubaliano hayo ni hatua muhimu kuelekea
kuondoa wasiwasi wa shirika la IAEA kuhusu mpango huo na
kuwafungulia mlango wachunguzi wake kuvitembelea vinu vingine
viwili vya nyuklia; kinu cha Arak na kinu cha urutubishaji wa madini
ya urani cha Gachin. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran akiwa na mkuu wa shirika la nguvu za atomiki la Iran, Ali Akhar Salehi, Mkurugenzi wa shirika la IAEA, Yukiya Amano, amesema makubaliano hayo yatafuatiwa na utekelezaji wa hatua muhimu katika miezi mitatu ijayo.
Amano ameyaeleza makubaliano hayo kuwa hatua muhimu, lakini akasisitiza bado kuna kazi kubwa ya kufanya.
