KANDORO: TAFUTENI MSHAURI WA HALMASHAURI


MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameishauri Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mkoani hapa kutafuta mshauri wa kifedha ili kupanua mapato ya halmashauri hiyo.

Ushauri huo ulitolewa Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa Kandoro akiwa na mkaguzi wan je waserikali wa mkoa wa Mbeya, Jane Venans wakati wakipitia matumizi ya fedha za Halamashauri hiyo.

Kandoro alisema kuwa Halmashauri inatakiwa kutafuta msauri wa kifedha wa Halmashauri ili kuibua vyanzo vya kifedha katika Halmashauri.

Alisema kuwa Halmashauri kama itakuwa na mshauri ambaye anaubunifu itafanikiwa kupata fedha mbalimbali za kuendeshea bahalimashauri.

“Nashauri mtafute mshauri wa kifedha wa halmashauri ili muibue miradi katika Halmashauri yenu ili muibue miradi na vyanzo vya fedha na kuongeza mapato” Alisema Kandoro.

Alisema kuwa kwa kufanya hiyo Halmashauri itajiendesha yenyewe na kujenga miradi ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wake.

Aliongeza kwa kuwataka madiwa kuwa wakali kwa watendaji ambao wanawatilia shaka na matumizi ya fedha za maendeleo ya wananchi wao.

Alisema kuwa madiwani wahakikishe mapato yanavyo ongezaka ndivyo matumizi yaonekane katika Halmashauri yao.

Kwa upade wake mkaguzi wa ndani wa Serikali Jane Venans aliitaka Halmashauri kupitia watendaji wake kuweza kujikita katika kuendeleza Halmashauri yao.

Alisema ili kufanikiwa ni kudhibidi mapato ya Halmashauri, kitu kitakacho isaidia Halmashauri kusonga mbele kimaendeleo.