MWENYEKITI wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema Freeman Mbowe amewataka wakazi wa
Mbeya kutuma maoni ya katika na kuwekea mkazo suala la maji kuwemo katika
katiba mpya.
Alisema kuwa katiba mpya iweke suala la kuwapatia
maji lewemo katika katika na iwe ni lazima kwa kiongozi atakaye kuwa madarakani
kuwapatia maji wananchi.
Aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhala mkoani
Mbeya na kuwataka wakazi hao kuliweka suala la maji kuwa ni haki ya msingi kwa
kila mwananchi.
Alisema kuwa kiongozi yeyote atakaye ingia
madarakani kuhakikisha wananchi wote wanapata maji na itakuwa ni kama sheria
likiwekwa katika katiba.
“Ni aibu kwa nchi kama hii iliyo zungukwa na maji
kila kona lakini kuna wananchi hawana maji na katika Afrika nzima nchi pekee ya
Kongo ina maji kwa wananchi wote na kwa Tanzania amboyo emezungukwa na maziwa
na mito kuna wananchi hawana maji” alisema Mbowe.
Aliongeza “Hata kama Chadema ikiwa madarakani au CCM
ama chama chochote kikishika dora lazima kiweke mbele suala la maji kwa kila
mwananchi”
Alisema kuwa wananchi bado wananafasi ya kutoa maoni
ya kuchangia katika maoni ya katiba kupitia chama chao kwa kutuma maoni kabla
ya kufika Augosti 31 ambapo itakuwa mwisho wa kupokea maoni kwa tume ya katiba
mpya.
Aliongeza kuwa Chadema inazunguka nchi nzima
kukusanya maoni ya wananchi ma kupeleka maoni hayo katika tume ya katiba.