MBOWE: "CCM IMEFIKA MWISHO KATIBA MPYA"

  • ASEMA ZANZIBAR WAOMBA SERIKALI TATU 
 
 
  • ZANZIBA WANAWABUNGE WENGI KULIKO WANANCHI WA ZANZIBAR UKIWEKA MZANIA 
 MWENYEKITI wa Chama Cha Demokreasia na Mbaendeleo (Chadema) Taifa Freeman Mbowa amesema chama cha mapinduzi (CCM) kimefikia ukomo wake kufuatia katiba mpya ambayo rasimu yake imetolewa na tume ya katiba hivi karibuni.

Akizungumza na wakazi wa kata ya Iyela jijini Mbeya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa kata ya hiyo ambao unatarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu.

Alisema kuwa kufuatia muunda wa katiba inayo kuja CCM inaelekea kufa kutokana na katiba hiyo kuruhusu mgombea binafsi na Serikali tatu.

Alisema kuwa uongozi sio jambo la kugombania viongozi wa chama hicho wanataka kuingia madarakani kuwa malengo ya kujipatia mali na uogozi wameweka kama kitega uchumi katiba mpya itawakata makali.

Alisema kuwa viongozi wa chama hicho wamekuwa wakila fedha za walipa kodi wakiwa madarakani na ndiyo maana wamekuwa wakiutafuta uongozi kwa kasi kubwa.

Alisema kuwa Katiba mpya imekuja kufuatia mkandamizo wa chama hicho ambapo walipo ingia bungeni siku ya kwanza alipokuwa akifungua buge la msimu huu Rais Jakaya Kikwete walitoka nje ya bunge kudai katiba mpya ambayo itatungwa na watanania wenyewe.

Alisema kuwa katika hii iliombwa kufuatia katiba ya zamani kuwa katiba kandamizi kwa watanzania na kuwa nyima haki zao za msingi na kuwa ni kandamizi.

Alisema kuwa katiba hii itaruhusu Serikali tatu ni kutokana na maombi ya wananchi wa Zanzibar wenye wabunge wengi kuuliko wakazi wa Tanzania bara.

Alisemakuwa Zanzibar wanataka uhuru kutokana na kuwa wamebanwa na katiba ile ya zamani nah ii itawapa uhuru kutoka na kuwapo kwa Serikali tatu.

“Serikali tatu italeta Uhuru kwa wakazi wa Zanzibar ambao wanabanwa na muungano serikari hizo zitawaweka wakazi hao huru kuliko ilivyo kuwa ile ya awali,” alisema Mbowe.

Aligusia maandamano ambayo walitakakuyafanya baada ya kutoka kwa matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012 yalihahilishwa kutokana  na kuwapo kwa ugeni wa Rais wa China hapa Nchini.

Alisema kuwa pesa ambazo zilichangishwa katika kipindi hicho kwa wananchi hazikutumika na sasa inatumika katika uchagunzi mdoko unaotarajiwa kufanyika katika kata 26 kote nchini.

Alisema Chadema inatarajia kuchukua jumla ya kata 20 kati ya kata 26 ambazo zitakuwa na uchaguzi mdogo Juni 16 hapa nchini ikiwemo na kata ya Iyela ya jijini Mbeya ambayo chama hicho0 kime msimamisha Charles Mkela kuitwaa kata hiyo.

Kwa upande wake mgombea wa uduiwani kata hiyo Charles Mtela alisema kuwa akifanikiwa kuchaguliwa katika uchaguzi huo atahakikisha kata hiyo inapata hospitari soko na huduma zingine za kijamii pamoja na barabara.