AKATWA NA MAPANGA KISA UCHAWI


MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Mbebe Wilayani Ileje Mkoani Hapo Wilson Mlwafu (68) ameuawa kwa kukatwa na upanga sehemu mbalimbali za mwili kwa tuhuma za ushilikina.

 Tukio hilo limetokea limetokea February 2 mwaka huu majira ya saa 3:30 usiku ambapo marehemu alikuwa anatoka kirabuni kunywa pombe za kienyeji na kukutana na kundi la vijana walio anza kumshambulia.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Senyamule alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu huyo alikuwa anatuhumiwa na watoto wake kuwa anafanya mambo ya kichawi jambo ambalo halina uhakika.

 Rosemary alisema kuwa serikali ya Tanzania haiamini masuala ya kishirikina hivyo aliwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi na kudai kuwa iwapo mtu atabainika kufanya hivyo sheria zitachukuliwa juu yake.

 Serikali yetu haiamini masuala ya uchawi na kuwa watu wamekuwa wakisema mara kwa mara kuhusu uchawi na mambo yanatokea ya mauaji kwa wingizaidi na tumekuwa tukishuhudia watu wakiuawa kwa tuhuma kama hizo za ushrlikina” alisema Senyamule.

Senyamule alisema kuwa marehemu alikatwa na upanga sana sehemu za kichwani na kuwa alikufa papo hapo kwa kuwa alikuwa amelewa pombe na watu waliofanya unyama huo walichukua nafasi hiyo ya kumvamia na kumuua.

 Alisesema wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji kama huyo na kuwa inatishia amani kwa wananchi kuwa wanaweza kuuliwa pasipo kuwa na ukweli kwa madai kuwa ni washirikina.

Mkuu huyo aliongeza kuwa upelelezi unaendelea wa tukuio hilo kwa kuwa chanzo bado hakijafahamika vizuri na kuwa jeshi la polisi linafanya kazi ya kuwatafuta walio fanya unyama huo na kuwa wananchi watoe ushirikiano katika suala hilo.