![]() |
| KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI |
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani wakati akifungua Klabu ya marafiki maarufu kama Friends club ya jijini Mbeya hivi karibuni katika ukumbi wa Mbeya Peak, alisema kuwa wale wote ambao wamejenga mazoea kuwa uhalifu ndio chanzo chao cha mapato sasa imefika mwisho.
Athumani alisema kuwa amekuja kwa kasi mpya na kupambana na waharifu wa aina yoyote ile kwa kushirikiana na jamii wakiwemo vijana ambao wako katika vikundi na Klabu mbalimbali kikiwemo cha friends Club.
Alisema vijana wananafasi kubwa katika kuionyesha Tanzania uwezo wao katika uwekezaji wa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo bioashara na zingenezo.
"Mahali palipo na amani na utulivu ndipo maendeleo yana weza kutokea na hakuna nchi yenye vurugu ikaendelea na wawekezaji wanataka kuwekeza sehemu yenye amani," alisema Athumani
Amani ikiwepo hata wawekezaji wanaweza kutiririka katika kuwekeza katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kusababisha nchi inakuwa katika nafasi nzuri ya maendeleo.
Aidha ametoa wito kwa vijana kuachana na siasa kwani siasa inawapotezea vijana muda mwingi wa maendeleo na kusababisha kukaa vijiweni kujadili vyoma na kuacha kijishughulisha kikamilifu.
"Nashukuru kama Klabu yenu haina chama chochote chasiasa na kufungamana na upande wowote wa dini na kukusanya vijana wa aina zote walio na elimu na wasio na elimu ni jambo zuiri litakalo wasaidia kusonga mbele kinaendeleo," Aliongeza Athumani
Awali vijana katika risara yao walisema kuwa watajitahidi kushirikiana na jeshi lapolisi katika kupambana na maovu katika jamii na kuwa klabu yao ya Friends Club haifungamani na upande wowote na wala dini yoyote.
Katika risara hiyo vijana wamejipanga kupambana na umasikini kwa kufungua miradi mbalimbali itakayo wasaidia kukwamuana wao kwa wao katika kukopeshana pesa za mitaji kutoka katika mfuko wa klabu.
Nae mratibu wa klabu hiyo, Freddy Jackson alisema kuwa wamejipanga kupambana na uharifu wowote na kushirikiana na jeshi hilo kwa umakini.
Jackson aliongeza kuwa wapo katika mpango wa kusajili klabu hiyo na klabu hiyo kwa sasa ipo chini kipindi cha Night Doctors kinachorushwa na kituo cha radio Mbeya Fm ya Jijini Mbeya kinachoruka kila siku ya Jumata Hadi Alhsmisi kuanzia saa 10:00 Usiku.

