JESHI
la Polisi Mkoani Mbeya limewataka wakazi wa Tunduma kuacha kujiingiza katika
maandamano yasiyo na tija kufuatia uvumi ulionezwa kuwa barabara kati ya Mwaka
na Tunduma yenye umbali wa kilometa mbili ahaitojengwa.
Katika taarifa yao mapema leo
asubuhi kwa vyombo vya habari imesema kuwa barabara hiyo haipo chini ya
mamalaka ya mji mdogo wa Tunduma bali ipo chini ya TANROADS hivyo kwenda kwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji huo ni makosa.
Hayo yanajiri kufutia uvumi kuwa leo
kutakuwa na maandamano kwa wakazi wa Tunduma na vitongoji vyake kupinga hatua
hiyo ya kutoijenga barabara ya Mwaka hadi Tunduma hali ambayo ingeendeleza ajali
katika eneo hilo.
Hata hivyo kuna taarifa zisizo rasmi
kwamba Diwani wa eneo hilo kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa vuguvugu la
maandamano hayo na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
