BAADHI ya wakazi wa kata ya Swaya Halmashauri ya Mbeya
Mkoani hapa wameiomba Serikali kuwafanyia fufumbuzi wa tatizo la maji katika
katayao ambalo limekuwa kelo katika Kata yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Elimtaa wamesema
wamekuwa wakipata shidi ya kufuata maji kwa zaidi ya kilomita mbili kutoka
katika makazi yao wakati wa kipindi cha kiangazi licha ya mradi wa maji
unaotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni chanzo chake kuwa katika kata hiyo.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Bw. Suto Julius amesema kuwa wananchi wa kata hiyo hasa wanawake
wamekuwa wakifuata maji kwa umbali wa zaidi ya kulomita mbili kotoka katika
kata hiyo.
Amesema wanawake wamekuwa wakitumia mda mwingi wa
kufanyamaendeleo katika harakati za kutafuta maji.
Mmoja wa weakazi wa kata hiyo Bi. Sabet Ntokani amesema kuwa huwawanapata shida sana kwanyakazi
za kiangazi kwa kufuata maji kwa umbali mrefu kutoka katika makazi yao na
kuteka maji yaliyo tuama hayo katika mto Swaya.
