UTALII TANZANIA: UKIJANI WA KUVUTIA KATIKA MBUGA YA SELOUS


Picha hizi zilipigwa tukiwa njiani kurudi campsite baada ya kumaliza mizunguko (game drive) ndani ya pori la akiba la Selous. Ukiwa unatoka kuelekea Kijijini (Mloka) utapita mahali ambapo ndio mpaka wa game reserve na eneo la kijiji.


Hii sio njia inayotumiwa na wageni bali ni njia ambayo inatumiwa na wahifadhi kufanya ukaguzi wa mipaka ya hifadhi. Kimsingi, barabara hii ni sehemu/alama ya mpaka wa pori la akiba. Upande wa kulia wa Barabara ni Pori la Akiba wakati upande wa kushoto wa barabara ni eneo la Kijiji cha Mloka.



 


KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA