Showing posts with label YALIYOJIRI HIVIKARIBUNI NYANDA ZA JU KUSINI 3. Show all posts
Showing posts with label YALIYOJIRI HIVIKARIBUNI NYANDA ZA JU KUSINI 3. Show all posts

YALIYOJIRI 2013: SHEHENA ZA VIPODOZI FEKI ZAKAMATWA MKOANI IRINGA



 Baadhi ya shehena za vipodozi  zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani  Iringa katika makao makuu ya jeshi hilo jana.(picha na Denis Mlowe)


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata shehena ya vipodozi vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi iliyokuwa inasafirishwa kutoka nchini Zambia kwenda jijini Dar es Salaam vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.

Shehena hizo zilikuwa zimebebwa na gari aina ya lori la mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP na tela lenye namba usajili T 598 BMK mali ya World Oil Ltd ya jijini Dar es Salaam.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya vipodozi ni  Dereva wa lori Mohamed Sadru(23) na Kassimu Kaifa anayesadikika ndio mwenye mali.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi  amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kusema kuwa walipata taarifa za kiitelejensia kutoka Tunduma kuwa kuna lori linasafirisha shehena hiyo kutoka nchini Zambia.

Mungi alisema walijiweka tayari kulikamata gari hilo kwa kukaa barabara kuu kuanzia saa moja jioni hadi ilipofika saa kumi alfajiri ndipo gari lilipofika na kukamatwa.

Anaongeza kuwa maafisa wa polisi mkoa wa Iringa walijipanga vizuri kuweza kulikagua gari hilo na waligundua kuna shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na TFDA na kuwaweka chini ya ulinzi dereva na roli hilo.

“Cha kushangaza gari la mafuta kuweza kubeba  vipodozi hivi vilivyopigwa marufuku hivyo tukaamua kuwashirikisha wadau wengine ambao ni TRA, TFDA na Tanroad kuweza kubaini makosa ambayo watuhumiwa hao wamefanya katika usafirishaji wa shehena hiyo.” Alisema Mungi

Mungi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha shehena hiyo ina thamani kubwa na ndio maana watuhumiwa walikuwa wanasafirisha kwa njia ya magendo na wanaendelea kuchunguza kubaini thamani halisi ya mzigo huo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mamlaka wa Chakula na Dawa (TFDA) mkoa wa Iringa, Deodata Rukupwa alisema shehena iliyokamatwa asilimia 100 ina kemikali iliyopigwa marufuku ya Hydroqunone na mamlaka hiyo.

Alisema vipodozi hivyo vitateketezwa kwa pamoja na jeshi la polisi na gari hilo kutaifishwa na serikali kutokana na kubeba mzigo wa magendo.

Rukupwa aliwataka wananchi kuwa makini katika kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na serikali na kutoa taarifa wanapobaini kuna vipodozi vilivyopigwa marufuku vinauzwa.
Na Denis Mlowe,Iringa
kwa hisani ya Pamoja blog
BABU MBARONI KWA MAUAJI YA MJUKUU

BABU MBARONI KWA MAUAJI YA MJUKUU


JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikila Zenobi Lusale (65) Mkazi wa Kijiji cha Sibwesa Tarafa ya Karema Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumuua mjukuu wake kwa kumpiga na fimbo kichwani baada ya kumtuhumu kumwibia debe moja la mahindi.
Kwa mijibu wa Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Joseph Shilinde tukio hilo lilitokea jana saa 11 jioni katika kitongoji cha Senta Magogo Kijiji cha Simbwesa Tarafa ya Karema Wilayani hapa. 
Kaimu kamanda Joseph Shilinde alimtaja aliyeuawa kwa kupigwa na fimbo kichwani na babu yake kuwa ni Stansilaus Joseph (15) Mkazi wa kijij hicho. 
Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa Zenobi alikwenda kwa jirani kunywa pombe ya kienyeji aina ya komoni nyakati za mchana na kisha aliporejea nyumbani kwake ambako alikuwa akiishi na mjuukuu wake huyo na ndipo alipo mwita kwa lengo la kufanya nae mazungumzo. 
Kaimu Kamanda huyo alieleza kuwa wakati wakiwa kwenye maongezi ndipo mtuhumiwa alipoanza kumshutumu mjukuu wake kuwa kuna mahindi debe moja yameibiwa ndani na yeye marehemu ndiye aliyeiba mahindi hayo Marehemu baada ya kuambiwa hivyo alikataa kuwa yeye hajaiba mahindi hayo labda aliuza mwenyewe na amesahau kama alimuuzia mtu kwani yeye hana tabia ya wizi. Inaelezwa kuwa baada ya kuelezwa hivyo mtuhumiwa alianza kumshambulia mjukuu wake kwa fimbo kichwani ambapo alipiga mayowe na ya kuomba msaada na huku akimsihi babu yake asiendelee kumpiga lakini hakufanya hivyo aliendelea kumpa kichapo na ghafla alianguka na kufariki dunia papo hapo. 
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upepelezi wa awali kukamilika. 

Kategori

Kategori