Showing posts with label Picha. Show all posts
Showing posts with label Picha. Show all posts

EFM yaendelea kugawa Ndinga Dar

EFM REDIO YAENDELEA NA SHINDANO LAKE LA SHIKA NDINGA,WIKI HII ILIKUWA WILAYA YA ILALA

Meneja Mkuu wa Efm redio, Denis Sebo akiwa katika picha ya pamoja na washidi wa shindano la shika ndinga walioshinda pikipiki kwenye viwanja vya Jica Shule Ilala jijini Dar es salaam. Kulia ni Zainabu Mhagama na kushoto ni Said Abdallah.
Washiriki wa Shindano hilo wakiendelea kushindana kwenye viwanja vya Jica Shule Ilala jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Efm redio, Denis Sebo akiwatazama washiriki wa kwenye viwanja vya jica Shule Ilala jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa kipindi cha uhondo Adam Melele a.k.a Swebe Santana wa Efm redio akimkaribisha Meneja wa Mauzo wa Star Times, Juma Mchina Sharobaro ili atowe zawadi kwa washindi wa tatu na wa pili kwenye viwanja vya jica Shule Ilala jijini Dar es Salaam.
.Meneja wa Mauzo wa Star Times, Juma Mchina Sharobaro akiwa na washiriki wa shindano hilo mara baada ya kuwapatia zawadi, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Vodacom Materi Mushi akiwakatika picha ya pamoja na washiriki wa shindano hilo mara baada ya kuwapatia zawadi, jijini Dar es Salaam.
Watu wa huduma ya kwanza wakiwahudumia washiriki wa Shindano hilo
Wananchi wa wakifatilia mashindano hayo kwenye viwanja vya jica Shule Ilala jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

UCHAGUZI LUDEWA MWANZO MWISHO


 Baadhi ya wananchi walio jitokeza kupiga kura Siku ya Jumapili jimbo la Ludewa licha ya kuwa wachache
 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa William Waziri akitangaza matokeo ya uchaguzi jimbo la Ludewa na kumtangaza mbunge mteuliwa Deo Ngalawa kuwa mbunge mteuliwa
 Deo Ngalawa akishangilia ushindi alioupata pembeni kulia ni mama wa Ngalawa akiungana na mwanae kushangilia ushindi
 Ilikuwa ni majira ya saa Mbili matokeo yakitangazwa cheti kinaonyeshwa kwa walio shuhutia matokeo yakitangazwa
Ngalawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa na kuwataka wakazi wa jimbo hilo kuona makubwa kutoka kwake.
(picha ni kutoka Ludewa na Mnyalu)
stori yake tafadhari BOFYA HAPA

VIONGOZI WA UTUMISHI KATIKA VIAPOVYWA UMAMINIFU

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Mathew Kirama fomu maalum ya kuweka Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma mapema leo ofisini kwake.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akielekeza namna ya kutoa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma zoezi lililofanyika mapema leo Ofisi ya Rais-Utumishi jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu akitia saini fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kulia) ofisini kwake mapema leo.
 Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakila kiapo cha  Uadilifu kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) mapema leo

PICHA; DAR KATIKA UBORA WAKE NA VIJIMAMBO



 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa muendesha Bajaji akivunja sheria kwa kupita pasipo ruhusiwa kupita, hii ni pamoja na kuharibu miondo mbinu ya Barabara ya  mabasi yaendayo haraka ya Morogoro jijini Dar es Salaam.
Madereva wa magari haya mambayo yameshindwa kupishana kwa usahihi  wakielewana mara baada ya kugongana leo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kama walivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.
 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa madereva wasiopenda kuvaa kofia ngumu(Herement) pamoja na Serikari Jeshi la Polisi kutoa agizo la kuvaa kofia hizo lakini wamekuwa wakiakipuuza sheria hiyo. wakingoja ningejua ninge.......
Mchana huo marekebisho ya hali ya tumbo yakiendelea katika sehemu ya chakula kama ilivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

Kategori

Kategori