Showing posts with label March 16. Show all posts
Showing posts with label March 16. Show all posts
Historia ya Rais Ahmed Ahmed alivymaliza utawala wa miaka 29 wa Issa Hayatou, CAF

Historia ya Rais Ahmed Ahmed alivymaliza utawala wa miaka 29 wa Issa Hayatou, CAF

Rais mpya wa shirikisho la Soka barani Afrika, Caf, Ahmed Ahmed.performgroup
Shirikisho la soka barani Afrika, Caf, hatimaye limepata rais mpya baada ya Ahmed Ahmed kuchaguliwa kwa kishindo na kumuangusha Issa Hayatou, moja ya viongozi wakongwe zaidi waliowahi kuhudumu kwa muda mrefu kwenye taasisi ya soka.
Ahmed amemshinda Hayatou kwa kura 34 kwa 20 katika uchaguzi ambao sasa unamaliza miaka 29 ya utawala wa Hayatou aliyekuwa akiongoza shirikisho hili la mpira barani Afrika toka mwaka 1988.
Ahmed, mwenye umri wa miaka 57 na baba wa watoto wawili, amekuwa kwa muda akifundisha soka na kucheza mpira kwa nyakati tofauti kabla ya kuchukua urais wa chama cha soka cha Madagascar mwaka 2003.
Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa wa kihistoria kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Issa hayatou kupata upinzani mkali ukilinganisha na chaguzi nyingine zilizotangulia ambapo mara zote amekuwa akipitishwa kwa kishindo na wakati mwingine kukosa mpinzani.
Toka kutangaza kuwa atawania kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka huu, Ahmed alipata mara moja uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya viongozi wa mashirikisho ya soka barani Afrika, ambao walipenda sera za mgombea huyu aliyekuwa akijinasibu kufanya mabadiliko makubwa kwenye shirikisho hilo la kulibadili soka la Afrika.
Mwaka huu mara kadhaa imeshuhudiwa Issa Hayatou akiingia kwenye mvutano wa maneno na marais wa vyama vya soka toka nchi za kusini mwa Afrika COSAFA, ambao wao toka awali waliweka wazi msimamo wao kuhusu kumuunga mkono Ahmed Ahmed.
Na ni mwanzoni mwa juma hili tu baada ya kuanza kwa mkutano mkuu wa Caf, Issa Hayatou kupitia kamati ya utendaji waliridhia kwa kauli moja kuanza kusikiliza shauri la kinidhamu dhidi ya rais wa chama cha soka cha Zimbabwe, Phillip Chiyangwa, aliyeitisha mkutano wa marais toka nchi za COSAFA kujadili namna ya kumuondoa Issa Hayatou madarakani.
Uchaguzi wa mwaka huu pia umekuwa na mvuto wa aina yake, kwakuwa hata baadhi ya vyama vya soka ambavyo kwa miaka nenda rudi vimekuwa vikimuunga mkono Issa Hayatou kwenye chaguzi zilizopita, walibadili kibao na kutangaza hadharani kutomuunga mkono.
Kwanini Issa Hayatou ameshindwa?
Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kuwa kushindwa kwa Hayatou huenda kusitokane sana na sera zake kwa soka la Afrika, lakini kikubwa ni kutokana na ukweli kuwa amekaa madarakani kwa muda mrefu na wengi walianza kumuona kama mtawala wa kiimla kwenye shirikisho hili.
Kingine ambacho wachambuzi wa mambo wanaona kilimuangusha Issa Hayatou ni kutokana na ukaribu wake na aliyekuwa rais wa shirikisho la mpira duniani Fifa, Sepp Blatter ambaye anatumikia adhabu ya muda wa miaka 6 kutojihusisha na soka kutokana na ubadhilifu alioufanya wakati akiwa kiongozi.
Kwenye uchaguzi uliopita wa fifa, Issa Hayatou pia hakuonekana kumuunga mkono rais wa sasa Gianni Infantino, ambaye majuma mawili yaliyopita alifanya ziara kwenye nchi kadhaa za Afrika ambazo kwa sehemu kubwa zilimuunga mkono na kumpigia kura.
Kwanini Ahmed Ahmed ameshinda?
Ahmed Ahmed, mgombea ambaye awali alikuwa hapewi sana nafasi ya kumshinda Hayatou kwenye uchaguzi wa mwaka huu, alipata umaarufu na uungwaji mkono toka kwa baadhi ya viongozi wa soka baada ya kuonekana kuwa na ahadi muhimu ya kulibadili soka la Afrika.
Ahmed anayeoonekana kuwa mwanamabadiliko ndani ya Caf, ameahidi kufanyia marekebisho baadhi ya vifungu vya katiba ya Caf ambavyo kwa sasa vinampa madaraka makubwa rais.
Mbali na marekebisho ya katiba, Ahmed aliahidi kubadili baadhi ya mifumo ya uendeshaji wa mashindano makubwa barani humo, huku akiahidi kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwaajili ya maendeleo ya soka barani Afrika.
Licha ya kuanguka kwa Issa Hayatou kwenye nafasi yake, kiongozi huyu aliyeingia madarakani toka mwaka 1988, amefanya makubwa kwenye soka la Afrika, ikiwemo kupanua wigo wa mashindano ya Afrika na kupata makampuni makubwa yanayifadhili mashindano hayo.
Issa Hayatou pia amesaidia vyama vingi vya michezo barani Afrika kuwa na uwezo wa kujitegemea na pia kulifanya soka la Afrika kutambulika kimataifa ikiwa ni pamoja na kuliwezesha bara hilo kupata timu tano kwenda kwenye mashindano ya kombe la dunia.

from Blogger http://ift.tt/2mO6DX3
via IFTTT


WANANCHI WAVUNJA VYOO VYA SHULE YA MSINGI HUKO NJOMBE

VYOO vya shule ya msingi Ramazani vya zamani vimevunjwa na wananchi baada ya kuona vyoo vipya walivyo vijenga kwa nguvu zao havitumiki na wanafunzi wa shule hiyo ikisubiliwa kufunguliwa na mwenge wa uhuru kitu lilicho sababisha mwenyekiti wa mtaa huo na Diwani kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa mawili.
Walio hojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa mawili ni pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule Diwani wa kata ya Ramazani na mwenyekiti wa mtaa huo huku kukidaiwa kuwa aliye enda polisi ni mkuu wa shule kwa shinikizo la afisa elimu.
Wananchi wakizungumzia kubomolewa kwa vyoo hivyo wanasema kuwa wameamua kubomoa vile vya zamani kwa lengo la watoto wao kuanza kutumia vile vipya.
Wananchi wanasema kuwa wamechoka kuwatibu watoto wao magonjwa ya mara kwa mara kutokana na kuwa na vyoo hivyo.
Diwani na mwenyekiti wanazungumzia kilichowapeleka kuhojiwa na polisi mbele ya wananchi.
Polisi iliingia katika shule ya msingi Ramadhani kwa lengo la kushuhudia vyoo vilivyo bomolewa na wananchi ili wanafunzi kuanza kutumia vipya baada ya kuikabidhi kamati ya shule siku tatu zililizopita lakini havijaanza kutumiaka kukidaiwa kuwa mpaka mwenge wa uhuru upite kuzindua mwezi April Mwaka huu ndipo vianze kutumika.

from Blogger http://ift.tt/2mxvRr1
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2n3S8k6
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nsz1RW
via IFTTT


WATU WATANO HATARI WALIOWAHI KUISHI

Hapo zamani wawindaji, maharamia na wanajeshi waliheshimiwa sana katika jamii. Walisifiwa sana na walikuwa wakionekana kama mashujaa.
Baadhi ya mashujaa waliongoza majeshi, wengine waliwawinda wanyama hatari na wengine walitawala makasri kama maharamia.
1
Kama ungependa kujua Zaidi kuhusu baadhi ya wawindaji mashuhuri, wapelelezi na wanajeshi wa zamani, hii hapa ni orodha ya mashujaa watano waliowahi kuwepo.
1. Madame ching au Ching Shih, alikuwa ni mmoja wa maharamia aliyewahi kuiongoza bahari ya China katika karne ya 19. Madame Ching alianza kama mwanamke anayejiuza, lakini baadae aliolewa na haramia. Madame Ching pia ni mmoja kati ya maharamia wachache sana waliowahi kustaafu kutoka uharamia.
Haramia aliyemuoa Madame Ching alikufa katika tsunami na nafasi yake ilichukuliwa na mkewe. Aliivuruga bahari ya uchina na kushinda vita nyingi alizopigana. Alipigana dhidi ya himaya nyingi kupita kiasi ikwemo Ureno, Uingereza na nasaba ya Qing.
Aliyashinda majeshi mengi na himaya nyingi. Amewahi pia kumteka afisa maarufu Richard Glass Poole pamoja na mabaharia wengine saba mnamo mwaka 1809. Alipata msamaha mwaka 1810 na kufariki mnamo mwaka 1844 akiwa na umri wa miaka 69.
Alichukuliwa kuwa mmoja kati ya maharamia wanawake waliokuwa maarufu na wenye nguvu sana katika historia.
2. Leo Major, alikuwa mwanajeshi kutoka Ufaransa na Canada aliyepigana vita ya pili ya dunia. Ni raia wa Canada pekee katika historia aliyepokea tuzo mbili za “Distinguished Conduct” katika vita mbili tofauti.
Mwanajeshi huyu aliyejulikana sana na alipoteza jicho lake moja katika vita alipotupiwa bomu la mkono na alikuwa akifananishwa na haramia.
Mnamo mwaka 1945, Meja aliteka mji wa Zwolle kutoka kwa wanajeshi wa kijerumani na alipokea tuzo yake ya kwanza. Wakati wakifanya mipango ya upelelezi na Koplo Willie Arsenault, wanajeshi hawa wawili walipanga kuuteka mji. Willie aliuawa, lakini Meja aliendelea na mpango wake. Aliingia mjini kwa fujo huku akiipiga bastola yake kwa vurugu pamoja na kutupa mabomu ya mkono.
Wanajeshi wa kijerumani walidhani kuwa jeshi la Canada linaushambulia mji, wakakimbia. Siku hiyo Meja aliwakamata wanajeshi zaidi ya 1800 na kuwauwa wengi Zaidi. Aliipokea medali yake ya kwanza ya “Distinguished conduct” kwa ushindi wake wa kushangaza.
Meja aliipata medali yake ya pili ya “Distinguished conduct” wakati wa vita ya Korea kwa kupigana vita ya kwanza ya Maryang San, ambapo aliuteka na kuushikilia mlima muhimu.
3. Jack Churchill, ambae alijulikana pia kama “Mad Jack”. Churchill ambae alikuwa afisa wa jeshi la Uingereza, maarufu sana kwa kupigana vita ya pili ya dunia akitumia sime ya Kiskochi, upinde mrefu pamoja na mishale.
Huyu ni maarufu kwa wito wake uliosema kuwa “Afisa yeyote anaeenda katika kazi pasipokuwa na upanga wake basi huyo hajavaa vizuri.” Mwaka 1943, Churchill aliongoza wanajeshi kutoka Sicily akiwa na upanga wake ulioning’inia kwenye mkanda , upinde na mishale pamoja na filimbi yake mkononi.
Aliupiga mji na kuwateka wafungwa 42 na kurudi kuchukua upanga wake alioupoteza wakati wa mapambano. Ilipoisha vita ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945, Churchill hakuridhika hata kidogo, alinukuliwa akisema kuwa “kama siyo hawa Wamarekani, tungeiendeleza vita hii kwa miaka mwingine 10.”
4. Jim Corbett alikuwa mwindaji maarufu aliyekamata duma na chui wengi huko India katika miaka ya 1907 mpaka 1938.
Inasemekana kuwa amewahi kutega na kuwaua duma 19 na chui 14 waliokuwa wakiwadhuru watu katika kazi yake ya uwindaji. Corbett alikuwa pia ni Kanali wa Jeshi la Uingereza huko India. Amewahi kuitwa ili awaue chui waliokuwa wakiwawinda na kuwajeruhi watu.
Ameandika vitabu kadhaa kuhusu uzoefu wake wa kuwinda. Katika maisha yake ya baadae alikuja kuwa mpigapicha na mhifadhi. Pia alikuwa msemaji wa ulinzi wa wanyamapori nchini india.
5. Hugh Glass, huyu alikuwa mpelelezi na muwindaji maarufu wa Marekani.
Mwaka 1823, alishambuliwa na kujeruhiwa na dubu. Rafiki zake wakiwa na uhakika kuwa amekufa walimtelekeza porini.
Hugh Glass alinusurika na kutambaa zaidi ya maili 200 kuelekea eneo salama kwa muda wa wiki sita pasipokuwa na chakula wala silaha yoyote.
Inasemekana alinusurika kwa kula mizizi ya miti na mimea mbalimbali pamoja na matunda. Wakati wengine wanasema kuwa aliua na kula nyoka wenye sumu kali (rattlesnakes).

from Blogger http://ift.tt/2nsdnNR
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mTJAfa
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mxrgFt
via IFTTT


MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AWASILI KWENYE MKUTANO MJINI MBABANE, SWAZILAND

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane – Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.

Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.

Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.

Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Heshima kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march,16, 2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Swaziland alipowasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbabane – SWAZILAND.

from Blogger http://ift.tt/2mTy5EC
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nJwvD4
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nsociD
via IFTTT


Kategori

Kategori