Showing posts with label July 01. Show all posts
Showing posts with label July 01. Show all posts
Unaambiwa FIFA Bado Hawajaamini Kilichotokea Kwa Rais wa TFF Tanzania, Wameamua Kufanya Jambo Hili

Unaambiwa FIFA Bado Hawajaamini Kilichotokea Kwa Rais wa TFF Tanzania, Wameamua Kufanya Jambo Hili

Shirikisho la soka Duniani FIFA litatuma wajumbe wake kwa ajili ya kuja kufanya uchunguzi juu ya kinachoendelea ndani ya TFF, hatua hiyo ya FIFA imefikiwa baada ya viongozi wa juu wa TFF Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa kupandishwa kizimbani kusomewa mashtaka yanayowakabili ikiwemo utakatishaji fedha.
Makamu wa rais wa TFF Wallace Karia amethibitisha kupokea taarifa ya ujio wa wajumbe wa FIFA nchini kwa ajili ya kufanya kiko cha pamoja.
“Wenzetu wa FIFA wametupigia walihitaji namba zangu kwa hiyo tutaongea nao lakini pia tutafanya kikao cha kamati ya utendaji wakiwemo wajumbe wa FIFA ambao watatumwa ili tuweze kufanya tathmini jinsi hali ilivyo na kutoa maamuzi ili mpira uendelee na maisha yaweze kuendelea.”
“Tumeona tuwashirikishe wenzetu wa FIFA kwa sababu kuna hali ya sintofahamu imeanza kuwepo kwa hiyo ni vizuri kuangalia katiba ya TFF inazungumza nini na ikiwezekana tuende katika utaratibu mzuri kwa hiyo tutafanya kikao cha FIFA na tunategemea tukifanye Jumanne, kama Rais wetu atafanikiwa kupata dhamana tunatarajia awepo kwenye hicho kikao.”
“Baada ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutoa habari kuhusu Rais na Katibu kushikiliwa walipiga simu wakiwa na taarifa kwamba wote tuko ndani, wakamtafuta mtu ambaye katiba inamtaja kwamba atakuwa anaendeleza shughuli za ofisi, kwa hiyo wamepewa namba yangu nasubiri mawasiliano nao na wanataka kuja ili tuwe na kikao cha pamoja.”
“Katiba ya TFF inasema Rais anapokuwa hayupo, makamu wake ndio anaendea kuongoza vikao na kila kitu kama makamu pia hayupo, mjumbe wa kamati ya utendaji ambaye amekaamadarakani kwa muda mrefu atakuwa kiongozi wa taratibu zote.”
“Kikao chetu cha kesho leo tutaangalia ni jinsi gani tutaweza kumkaimisha ukatibu mmoja wa wafanyakazi wa hapa ili shughuli za taasisi ziweze kuendelea.”
Malinzi na Mwesigwa watapandishwa tena mahakamani Jumatatu Juni 3, 2017 ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya viongozi hao.

from Blogger http://ift.tt/2uvHRxQ
via IFTTT


Video: Heshima anayopewa Niyonzima Rwanda, tetesi za kwenda Simba pia zimewafikia

Dauda TV imekanyaga jijini Kigali, Rwanda, katika mishemishe za town ikafanikiwa kupiga story na dereva tax (Jimmy) wa mjini Kigali na kumuuliza juu ya habari za star wa Yanga na timu ya taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima.
Dereva tax anasema Niyonzima ni kipenzi cha wapenda soka wa Rwanda na wanamfuatilia sana hata akiwa Bongo katika timu yake ya Yanga ambayo tayari imetangaza kumuacha na i tetesi za Niyonzima kusaini Simba zimeshazungumzwa pia Rwanda.

from Blogger http://ift.tt/2uaW7ws
via IFTTT


JPM amuamshia Dude Boss wa Tantrade Kwenye Viwanja vya Sabasaba

JPM amuamshia Dude Boss wa Tantrade Kwenye Viwanja vya Sabasaba

Katika hotuba yake kwenye maonesho hayo Rais JPM amewaomba waandaaji na viongozi kuweka mipango ili kujenga Hotel na Majengo mapya katika viwanja hivyo akiwataka wajenge kiwanda kitakachowasaidia watanzania kupata ajira na kukarabati majengo kama yamechakaa.
“Haingii akili wao ndio wanatusisitizia mambo ya biashara na viwanda na theme ya mwaka huu inazungumzia kukuza biashara na maendeleo ya viwanda sasa wao badala ya kuzungumza juu ya maendeleo ya viwanda wanataka wajenge Hotel hapa, watengeneze majengo mapya sasa. Sijaelewa.
“Sasa kama hizo hela zipo basi mzipeleke mkajenge kiwanda cha mfano. Haya majengo yaliyopo ambayo mnayaona yamechakaa hawa wanaokuja kuonesha bidhaa zao wapeni bure wajenge ili kila mwaka wawe wanaonesha.
“Hiyo Hotel kwani mkijenga lazima walale hapa hapa? Mnaweza kujenga Hotel hapa bado wakaenda Hotelini mjini. Mimi nilifikiri ili kujenga jenga majengo fikirieni zaidi katika kujenga viwanda kwa ajili ya mfano wa kuonesha Wizara kweli iko mbele kwa kujenga viwanda.
“Haya majumba yanaweza yakawa siyo mazuri sana lakini ni mazuri kwa watu wa Tanzania ambao wanataka kuona bidhaa. Yanayowaleta hapa siyo majumba Watanzania wanakuja hapa kuangalia Tecknolojia na vifaa vilivyomo.
“Inawezekana mimi nipo tofauti mnisamahee lakini katika muelekeo wangu ninaona hizo hela mnataka kuzitumia vibaya. Mwenyekiti nimekuteua juzi umeshaanza kufikiria majengo hapa pamoja na Body yako mnanifanya nifikirie zaidi.
“Nimeshasema, nimewapongeza na ninawapongeza washiriki wote basi tuangalie masuala ambayo ni very positive kwa Taifa hili tunataka kuwa na viwanda vingi na siyo Hoteli nyingi.” Magufuli.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t2D5ty
via IFTTT


Breaking News: Mtangazaji wa Azam TV Apatikana

Breaking News: Mtangazaji wa Azam TV Apatikana

Mtangazaji wa Azam Tv Fatna Ramole aliyeripotiwa kutoweka tangu Juzi Alhamisi ameripotiwa na ndugu yake Lulu Remole.
Lulu amethibitisha kupitia Ukurasa wake wa Twitter na kuwashukuru waungwana walishirikiana kumtafuta Dada yake.
“Asante wote kwa ushirikiano wenu, Mungu mkubwa tumepata taarifa na tukaweza kumpata Fatna.Bila RT zenu nisingepigiwa na huyo Dada. Mbarikiwe” – Lulu
Lulu aliripoti na kuujuza umma kupitia mitandao ya kijamii kuwa Dada yake hajaonekana kwa muda wa saa 48.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tBnJxG
via IFTTT


Kategori

Kategori