Showing posts with label 2017 at 11:37AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:37AM. Show all posts

Imefichukaaa..Hii Ndio Sababu Kuu Amabyo Haisemwi Kuhusu Ujio a Waziri Mkuu wa Ethiopia…!!!

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajia kufanya ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini leo, Machi 31 na Aprili 1.
Ziara hiyo ni mwaliko wa Rais John Magufuli kwa Dessalegn kufuatia mazungumzo waliyoyafanya huko Addis Ababa, Ethiopia baada ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika (AU).
Akizungumzia ziara hiyo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba amesema baada ya kuwasili nchini, Waziri Mkuu huyo atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli na baadaye ujumbe wa Ethiopia na Tanzania watakaa pamoja na kuzungumza.
Dk Kolimba amesema viongozi hao watashuhudia utiaji saini mikataba mitatu katika maeneo ya biashara, uwekezaji, utalii na diplomasia.
“Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na kujadili fursa za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara,” amesema Dk Kolimba.
Siku itakayofuata, Aprili Mosi, Dessalegn atafanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam na baadaye siku hiyo ataondoka kurejea Ethiopia.
Dk Kolimba amesema Ethiopia imeonyesha nia ya kufungua ubalozi wake hapa nchini. Kwa sasa Ethiopia inawakilishwa nchini na Balozi wake aliyepo Nairobi, Kenya.
Dessalegn alitembelea Tanzania mwaka 2015 na kushiriki uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa za kuulia viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria. Pia, alishiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli zilizofanyika Novemba 2015.
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2npO2jL
via IFTTT


Harmonize Adaiwa Kumtukana Live Meneja wa Harmorapa Wakiwa Studio

Taarifa iliyotolewa na Kituo cha East Africa Television kupitia ukurasa wao wa Twitter imeeleza kuwa, Msanii kutoka WCB, Harmonize ilikuwa awepo kwenye kipindi cha FNL cha televisheni hiyo usiku huu, lakini ameingia mitini baada ya kumuona meneja wa msanii Harmorapa maeneo ya studio hizo.
Inadaiwa kuwa baada ya kumuona meneja wa Harmorapa, msanii Harmonize amemuoneshea kidole cha kati ambacho hudaiwa kuwa ni ishara ya tusi kisha akaondoka maeneo ya studio hizo.
Aidha Harmorapa amelaani kitendo hicho cha udharirishaji na kudai kuwa Harmonize amemtukana bosi wake kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha kati baada ya kukutana.
Kwa upande wao, kituo cha EATV, kupitia Twitter kimeomba msamaha kwa watazamaji wake wote kutokana na kitendo hicho cha aibu kilichofanywa na msanii huyo.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nyrf8i
via IFTTT


Kimenukaaa…Madaktari 500 wa Tanzania Wakataliwa Kenya,Madaktari wa Kenya Wasijisumbue Kutia Miguu Yao Kenya Wakikaidi Cha Moto Watakiona…!!!

UMOJA wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali hatua ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina madaktari wengi ambao hawaajiriwa.
Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kuwa Serikali ya Kenya haijawa makini katika kushughulika na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo
Akizungumza na mtandao wa The Star wa nchini Kenya siku ya Jumamosi, Oluga alisema
“Kenya ina zaidi ya madaktari 1,400 ambao wanasubiria ajira. Itakuwa gharama kubwa na dalili ya kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na madaktari 500 wa kitanzania kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku,” amesema.
Oluga amesema kuwa Kenya inapaswa kupitia upya utaratibu wake wa Rasilimali Watu kwa mujibu wa miongozo ya Afya kama ambavyo KMPDU imekuwa ikihitaji hapo kabla.

from Blogger http://ift.tt/2nr3Upl
via IFTTT


Kategori

Kategori