Showing posts with label 2017 at 11:36AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:36AM. Show all posts
Wananchi watangaziwa Msiba Feki, Wachimba Kaburi la Mtu aliyehai

Wananchi watangaziwa Msiba Feki, Wachimba Kaburi la Mtu aliyehai

Makubwa Haya!! Wananchi wa Kitongoji cha Bujinge,kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuchimba kaburi kisha kulazimika kufukia kaburi hilo la mtoto aliyedaiwa kufariki dunia.
Blog hii imezungumza na mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,Salum Juma,anasimulia ilivyokuwa:
“Kuna mama mmoja anaitwa Suzana Charles kwao ni Kizumbi lakini ameolewa huko Musoma,aliondoka Shinyanga akiwa na mtoto aliyezaa na mwanamme mwingine,juzi kapiga simu kwenye nyumbani kwao Kizumbi kuwa mtoto wake amefariki,na wanasafirisha mwili wa marehemu kutoka Musoma hadi Shinyanga,kama zilivyo taratibu za wananzengo tukaanza taratibu za kushughulika na msiba”,anaeleza Salum Juma.
“Jana tulihudhuria msibani nyumbani kwa marehemu Mzee Charles hapa Kizumbi,tukachimba kaburi,tukawa tunawasiliana naye akisema wapo njiani wanakuja,baadaye huyo mama akasema wamefika Misungwi Mwanza lakini gari yao imemaliza mafuta hivyo tuwatumie pesa,tukawatumia shilingi laki moja na simu yake haikuwa inapatikana tena”,anasimulia Juma.
“Baada ya kutuma shilingi laki moja,tukategemea kuwa safari inaendelea,tukaendelea na taratibu za mazishi tukiamiani kuwa mpaka saa tisa alasiri watakuwa wamefika Shinyanga,huwezi amini mpaka saa 12 walikuwa bado hawajafika,tukakubaliana kuwa kesho yake yaani leo tufike kwa ajili ya kuendelea na msiba”,
“Ilipofika saa nne usiku jana,Yule bwana aliyekuwa amemuoa huyo mwanamke akapiga simu anauliza mke wake kama amefika Shinyanga? Maana ametoka Musoma,tukamuuliza kuhusu msiba,akasema hana taarifa za msiba kwani mke wake ametoroka na mtoto akiwa salama”,
“Leo tumeamka tukaambiwa kuwa hakuna msiba wowote,hivyo nzengo tumedanganywa,na kaburi letu tulikuwa hatujalifukia tunaendelea kujadili,kidogo majira ya saa nne asubuhi leo Jumapili Yule mama akawa amewasili Kizumbi,Shinyanga akiwa na mwanae,amefika hapa kwao,tumempokea,tukaanza kumhoji kuhusu kilichotokea”,
“Tulipomhoji amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na matatizo ya kifamilia kule alikokuwa anasumbuliwa na maradhi hana pesa ya kumsaidia kupata matibabu,imefikia hivyo na sasa ndiyo tumemaliza kufukia kaburi”,anaeleza Salum Juma.
Imeandaliwa na Kadama Malunde-Malunde1 blog

from Blogger http://ift.tt/2sH6oit
via IFTTT


Shahidi Afunguka Mapya Kuhusu Scorpion Mtoboa Macho..Wengi Wapigwa na Butwaa Mahakamani..!!!

Shahidi Afunguka Mapya Kuhusu Scorpion Mtoboa Macho..Wengi Wapigwa na Butwaa Mahakamani..!!!

SHAHIDI katika kesi inayomkabili mshitakiwa Salum Njwete ‘Scorpion’, ya kuiba kujeruhi na kumtoboa macho Saidi Mrisho amedai mshitakiwa huyo ni mlinzi wa amani.
Katika kesi hiyo iliyoendelea kusikilizwa jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, shahidi huyo, Deus Magosa alidai anamfahamu hivyo mshitakiwa. 
Shahidi huyo mkazi wa Buguruni ambaye ni kiongozi wa ulinzi shirikishi wa eneo hilo, alidai kuwa yeye ndiye aliyempa ajira ya ulinzi wa amani mshitakiwa kwenye eneo hilo la biashara ndogondogo.
Mwendesha mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alimhoji shahidi huyo namna anavyomfahamu Scorpion ambapo mbele ya Hakimu Flora Haule, Magosa (46) alijibu anamfahamu kwani mshitakiwa aliajiriwa na wafanyabiashara wadogo kuwalinda pamoja na biashara zao pamoja na uongozi wao wa ulinzi ushirikishi.
Aliendelea kudai kuwa Salum alikuwa akilipwa Sh 10,000 kwa siku na wafanyabiashara hao kwa kuwawezesha kuendelea na biashara zao bila matukio ya wizi.
Hata hivyo, shahidi huyo alipoulizwa kama anakumbuka kilichotokea Septemba 6 mwaka jana, Magosa alijibu kwamba siku hiyo hakuwapo alikuwa msibani nje ya Dar es Salaam
Aliendelea kudai kuwa aliporudi alisikia watu wakizungumza mtaani, kwamba kuna mtu alitobolewa macho na kujeruhiwa katika tukio lililotokea maeneo ya Buguruni ambapo walimtaja mshitakiwa kuwa ndiye aliyehusika na tukio hilo.
Wakili alimwuliza baada ya hapo nini kiliendelea shahidi akajibu waliitwa Polisi na alipokwenda aliulizwa kama anamfahamu Salum Njwete ambapo alijibu anamfahamu na kumtaka akamwite.
Shahidi alidai alimfuata mshitakiwa na bila shaka wala kukataa alisema yeye ni raia mwema na alikwenda polisi bila kukamatwa na akaambiwa niondoke akamwacha mshitakiwa Polisi Buguruni.
Wakili Katuga alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Aprili 18 ushahidi utakapoendelea kutolewa.

from Blogger http://ift.tt/2n6vI32
via IFTTT


Hali Mbaya CCM Yawaliza Makatibu Wakuu…!!!

Viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro wamewataka makatibu wa matawi na mashina wa chama hicho kuachana na mpango wa kususia uchaguzi wa viongozi wa ngazi hiyo kwa madai ya kutokulipwa posho za kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake jana, Katibu wa Tawi la Luleni, Kata ya Tomondo, Salumu Waziri alisema kutokana na kudai posho hizo kwa muda mrefu ameamua kususia uchaguzi huo na tayari amekabidhi fomu za wagombea kwenye ofisi ya kata.
Waziri alisema chama hicho kilitoa fedha za posho na kumkabidhi kiongozi mmoja wa wilaya ambaye hakuwalipa.
Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge alisema chama hicho kilishatoa fedha za kuwalipa viongozi wa matawi na mashina kupitia kwa katibu wa wilaya hiyo.
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2og2Nt6
via IFTTT


Kategori

Kategori