Showing posts with label 2017 at 10:32AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:32AM. Show all posts
NGELEJA AELEZA SABABU ZA KURUDISHA FEDHA SERIKALI BADALA YA RUGEMARILA

NGELEJA AELEZA SABABU ZA KURUDISHA FEDHA SERIKALI BADALA YA RUGEMARILA

Siku chache baada ya kutangaza kuwasilisha shilingi milioni 40 katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amefafanua sababu za kutomrejeshea fedha huyo mfanyabiashara, James Rugemalira ambaye alimpa awali kama msaada.
Fedha hizo ni sehemu ya shilingi bilioni 306 zilizotolewa katika akaunti maalum ya Tegeta Escrow mwaka 2014 iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, fedha zizotolewa kimakosa wakati kesi ya mgogoro wa kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ikiwa bado haijatolewa maamuzi.
Kwa mujibu wa taratibu, fedha hizo zilipaswa kutolewa baada ya kesi husika kukamilika na pande zote mbili kukaa pamoja kukokotoa kiasi cha fedha ambacho kila upande ungepaswa kupata kwa mujibu wa maamuzi.
“Kwa mazingira halisi yanayomkabili aliyenipa msaada, mahali salama pa kurejesha hizo fedha sasa ni serikalini. Serikali itajua kuwa fedha hizo zinastahili kwenda kwa Rugemalira sasa au wasubiri hatima ya kesi,” Ngeleja anakaririwa na Gazeti la Mwananchi .
“Ningerudisha kwa Rugemarila watu wangeweza kuibua hoja kwamba labda napiga changa la macho tu,” aliongeza.
Mfanyabiashara huyo maarufu ambaye kampuni yake ya VIP Engineering ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya IPTL, pamoja na Mwenyekiti wa Pan African Power Solution (PAP), Harbinder Singh Seth wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na bado wako mahabusu.
Mgao wa fedha hizo pia uliwafikia Anna Tibaijuka aliyekuwa waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Andrew Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Methodiu Kilaini, Jaji John Ruhangisa na wengine.
-Mwananchi
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sSGLMe
via IFTTT


Baada ya Diamond Kuomba Suluhu Kwa Gwajima, Gwajima Asema..

Baada ya Diamond Kuomba Suluhu Kwa Gwajima, Gwajima Asema..

“Diamond Plutnumz ameepuka ugomvi na Bishop Gwajima. Big Up Diamond. Lakini jifunze zaidi, kwamba kukaa kimya wakati wa dhuluma ni dhambi kubwa. Ukumbuke zaidi kuwa, kama Mwalimu Nyerere na wale Wazee wangekaa kimya enzi hizo, hadi leo tungekuwa tunatawaliwa na Malkia Elizabeth na Si John Pombe Magufuli”.-Julius S. Mtatiro
Image may contain: text 
“Leo Ibada itakuwa LIVE on YOUTUBE kuanzia saa nne na nusu, kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Kibo Dar es Salaam. Link itakuwepo kwenye Bio yangu. Usikose”-Bishop Dr Josephat Gwajima

from Blogger http://ift.tt/2od7PnS
via IFTTT


Sumaye: Kama kweli Makonda Alifeli Kidato cha Nne, Simlaumu kwa Anachokifanya..!!!

Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, amesema kama yasemayo kuhusu elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni kweli, hamlaumu kwa maamuzi yake mbalimbali ambayo yamekuwa yakikosolewa vikali na wananchi.
Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii jijini Dar es Salaam, Sumaye alidai kuwa Makonda amepewa cheo kikubwa ambacho elimu yake haikimudu.
“Kama ni kweli [Makonda] amefeli darasa la saba kabisa, form four akafeli zote kabisa, kama ni kweli hivi ulitegemea afanyeje? Aendeshe mkoa sawa sawa?” alihoji Sumaye.
“Kama hizi failure ni kweli, huo uwezo wa kubeba hata wilaya uko wapi? Kwahiyo mimi simlamu Makonda. Yule bwana kwenye uongozi kuna kitu kinaitwa level of incompetency,” ameongeza.
Amedai kuwa huenda katika nyadhifa za chini Makonda alionekana kufanya vizuri hali iliyopelekea kupandishwa daraja haraka hadi kufikia kwenye kiwango ambacho hana uwezo nacho.
“Maana kama umefika mahali unavamia vituo vya habari, anakwenda waziri anayehusika na sekta hiyo anasikitika, anaeleza maelezo yale ambayo tumeyasikia sisi kwenye mitandao mengine mimi siwezi hata kuyarudia lazima kuna tatizo.”
Sumaye amesisitiza kuwa Makonda amefika mwisho wa uwezo wake.
Pia Sumaye amemshauri Rais Dkt John Magufuli kutii hisia za wananchi wake katika maamuzi anayoyafanya.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nLrjCw
via IFTTT


Mchungaji Gwajima Kuwafungukia Watangazaji wa Clouds TV leo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mchungaji Gwajima Ameandika Haya:
From @bishopgwajima – Nitatoa ufafanuzi wa wazi juu ya taarifa zinazosambazwa mtandaoni na baadhi ya watangazaji wa Clouds TV. Nitakuwa LIVE kwenye YouTube kuanzia saa nne na nusu asubuhi ya leo. Link ya channel ipo kwenye Bio yangu unaweza kusubscribe ili ujulishwe Mara niingiapo hewani. Mungu akubariki.

from Blogger http://ift.tt/2n305pf
via IFTTT


Kategori

Kategori