Showing posts with label 2017 at 05:39PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 05:39PM. Show all posts
Profesa Jay Afunguka Wema Sepetu Kuikacha Harusi yake

Profesa Jay Afunguka Wema Sepetu Kuikacha Harusi yake

BAADA ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu kuikacha harusi yake.
Taarifa za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria kwenye harusi hiyo.
“Unajua Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya Jay maana wangekuwa sawa ungeona mbwembwe zake ukumbini lakini hakutokea,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Profesa Jay kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa honeymoon ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Risasi Jumamosi: Hongera kwa kuoa na kuachana na ubachela Jay. Profesa
Jay: Asante sana, karibu.
Risasi Jumamosi: Kuna habari kuwa wewe na Wema mna bifu ndiyo maana hakuhudhuria hata kwenye harusi yako, hili likoje?
Profesa Jay: Jamani watu hawaishiwi maneno! Wema ni kamanda wangu tena tunahesh
imiana kwelikweli nisizuliwe bifu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Risasi Jumamosi: Kwa nini sasa hakuwepo au hukumwalika?
Profesa Jay: Mbona kuna watu wengi tu hawakuhudhuria kwa nini Wema? Mwacheni dada yangu apumzike, acha hizo stori. Profesa Jay kwa upande mwingine alieleza kuwa kesho Jumapili anatarajia kufanya sherehe kubwa kuliko ya mwanzo huko jimboni kwake Mikumi ambayo kila mwananchi atahudhuria kwani hakutakuwa na kadi na itafanyika uwanjani ikiwa ni shukrani kwao kwa kumchagua kuwatumikia

from Blogger http://ift.tt/2te6N0v
via IFTTT


Chatu mlevi alindwa na wafungwa Australia

Chatu mlevi alindwa na wafungwa Australia

Chatu huyo atapata makao mapya kesi itakapokamilika
Polisi wa Australia walipovamia mahabara moja mwaka uliopita, huenda walitarajia kupata madawa ya kulevya, vifaa vya kutengeneza dawa hizo na pesa nyingi .
Lakini msako wao ulifichua kitu chengine- chatu mwenye urefu wa futi sita ambaye alionyesha dalili za kulevya. Inadaiwa mafusho ya dawa hizo na chembe chembe zake zilikuwa zimemwingia mwilini kupitia ngozi yake.
Miezi saba baadaye, nyoka huyo aliyekuwa mwenye fujo sana amerejelea hali yake ya kaawaida akiwa chini ya ulinzi wa wafungwa 14 waliochaguliwa kufanya kazi katika programu ya kuwalinda wanyama pori.
Ni mmoja kati ya wanyama 250 ambao wanalindwa katika gereza moja mjini Sydney ambalo pia lina kangaroo, wanyama tofauti na ndege wa asili.
Gereza hilo la John Morony pia linawalinda wanyama wanaotambaa mbalimbali walionaswa katika misako ya polisi.
Kulingana na mmoja wa maafisa wa gereza hilo, kuna wahalifu ambao wanatumia nyoka walio na sumu kali kulinda bunduki na madawa yao ya kulevya.
Chatu huyo atapata makao mapya baada ya mahakama kukamilisha kesi dhidi ya washukiwa wa madawa ya kulevya yaliyomuathiri.
Gavana wa gereza Ivan Clader amesema programu hiyo ya kuwalinda wanyama kama hao imekuwa ikiendeshwa kwa miaka 20 sasa na imechangia pakubwa katika kubadilisha mienendo ya wafungwa.
“Tunachoona ni kuwa wanaume katika programu hii wanaopewa nafasi ya kuwalinda wanyama hawa, hubadilika na kuwa wenye utu na watulivu,” alieleza BBC.
“Kuwapa wafungwa fursa hii na majukumu ya kuwalinda wanyama kunachangia pakubwa katika programu ya kuwabadilisha tabia yao.”

from Blogger http://ift.tt/2ptL8uY
via IFTTT


TUCTA Yajipanga Kuipeleka Serikali Mahakamani

TUCTA Yajipanga Kuipeleka Serikali Mahakamani

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) limeitaka serikali kusitisha makato ya asilimia 15 kama malipo ya mkopo wa elimu ya juu na kurudi kiwango cha awali cha asilimia nane kinyume na hapo wataipeleka mahakamani.
Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema Baraza kuu la shirikisho hilo limesharidhia uamuzi huo na tayari lipo kwa wanasheria.


“Wanasheria wetu wanalifanyia kazi na kuendelea kukusanya nyaraka zitakazotusaidia,muda wowote kuanzia wiki Idaho tutalifikisha suala hili mahakamani,” alisema

Alisema ameendelea kupata malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi kutokana na makato hayo ikilinganishwa na hali ngumu ya maisha ilivyo sasa.

from Blogger http://ift.tt/2nEkTFD
via IFTTT


Rais Magufuli azidi kuiandama mitandao ya Kijamii..

Akiongea leo wakati anaapisha wateule wapya Ikulu. Amesema mitandao yetu ni ya ovyoovyo na inaandika mambo ya ajabu ajabu.
“Jana nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti Mwakyembe hawezi kuja kuapishwa, na mimi nilikuwa nasubiri asifike nione. ”Sasa si huyu hapa amefika”
Ameongeza kuwa….. “Jana kuna mwingine kapost Kinana kuongea na waandishi wa habari kesho, wakati ukweli Kinana nimemtuma India Kwa siku kumi na mbili”
Amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuzipa nafasi habari mbaya mbaya tu, “mfano kuna tv habari za migogoro ya wafugaji ndio wanaipa nafasi kubwa zaidi, amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.
Ameshangaa magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo.
Amemwambia Mwakyembe akasimamie kwa umakini hasa tasnia ya habari, amesema hayupo tayari kuona nchi ikichezewa..l
Ameshangaa kutangaza kutoandika habari za mtu, wakati huo huo wanaandika mbaya tu…. “Kama hamtaki kumwandika si masiandike yote mazuri na mabaya”
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nM4fDd
via IFTTT


RAIS MAGUFULI AFICHUA NJAMA YA BAADHI YA WABUNGE WA CCM KUMNGโ€™OA WAZIRI MKUU

RAIS MAGUFULI AFICHUA NJAMA YA BAADHI YA WABUNGE WA CCM KUMNG’OA WAZIRI MKUU

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa bado yupo mkoani Dodoma, jana alipata nafasi ya kufanya kikao na wabunge wa chama hicho ambapo alizungumza mambo mbalimbali ambayo hafurahishwi nayo kama kiongozi mkuu wa chama.
RG1A0483
Rais Magufuli alikutana na wabunge hao katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumza nao ni pamoja na kuwaambia kuwa anafahamu baadhi ya wabunge wanampinga Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Nafahamu baadhi yenu mnampinga Waziri Mkuu na mnataka aondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye, naomba niwaambie kuwa hamtafanikiwa. Mimi namuunga mkono msaidizi wangu huyuo kwa asilimia 100 kwa nimejionea mwenye namna anavyoweza kufanya kazi, alisema Rais Dkt Magufuli.
Hata mkimuondoa, nikija kuteua mwingine nitamleta huyu huyu na endapo mtamkataa basi nitavunja bunge wote mrudi kwenye uchaguzi.
Mbali na hilo kiongozi huyo alitoa onyo kwa wabunge wa CCM ambao wanagawa muda wao wa kuzungumza na kuwapa wabunge wa upinzani pindi wanapokuwa kwenye vikao vya bunge. Kauli hii imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Boniface Getere kumpa dakika tano mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba kutoka kwenye muda wake wa kuchangia ambao ni dakika 10.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Dkt Magufuli amewaambia kuwa anakerwa na baadhi ya wabunge kufifisha jitihada za serikali katika kupambana na dawa za kulevya huku akimtuhumu mbunge mmoja kutoa siri na kuzipeleka upinzani.
Kuhusu matangazo ya bunge kutokurushwa mubashara, Mwenyekiti wa CCM aliwaambia wabunge hao kuwa yeye ndio aliamua iwe hivyo kutokana na wabunge wengi kuwa wapiga porojo tu.
Kikao hicho kilichofanyika chini ya ulinzi mkali huku wabunge wakizuiwa kuingia na simu, kilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.

from Blogger http://ift.tt/2nnoPKg
via IFTTT


Kategori

Kategori