Showing posts with label 2017 at 04:40PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 04:40PM. Show all posts
PICHA-Chemical aamua kuwa dada du!!

PICHA-Chemical aamua kuwa dada du!!

Mwana dada chemical asiyekuwa na mpinzani kunako ulingo wa hip hop kwa upande wa kina dada tanzania ameamuwa kutoka kwenye utomboy na sasa amekuwa na muonekano wa beyonce. Inasemekana baada ya msanii mwenzake “stereo” ambaye anahit na wimbo wake wa “mpe habari” kumtoa bikra aliyokuwa akidai kuwa nayo sasa amebadilika kabisa kimuonekano. 

from Blogger http://ift.tt/2uelek6
via IFTTT


HUYU NDIYE RAIS WA KWANZA WA AFRIKA KUKUTANA NA RAIS DONALD TRUMP

HUYU NDIYE RAIS WA KWANZA WA AFRIKA KUKUTANA NA RAIS DONALD TRUMP

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi yupo, Washington, D.C nchini Marekani ambapo anatarajia kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump na kufanya naye mazungumzo.
Rais Abdel Fattah al-Sisi atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka barani Afrika kukutana na Rais Trump. Lakini pia, alikuwa ndiye kiongozi wa kwanza wa Afrika kuzungumza na kumpongeza Trump baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika Novemba 8, mwaka jana.
Masuala ya mgogoro kati ya Palestine na Israel yanatarajiwa kutawala sehemu kubwa ya mazungumzo yao, lakini pia masuala ya ugaidi duniani wakiegemea zaidi kupambana na kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu (ISIS).
Viongozi hawa walikutana Septemba mwaka jana jijini New York wakati Rais Sisi alipokuwa nchini humo kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN).

from Blogger http://ift.tt/2otjm54
via IFTTT


Ubovu wa stendi ya Mabasi Njombe yazua kizaazaa

Ubovu wa stendi ya Mabasi Njombe yazua kizaazaa

Madereva na watumiaji wa mabasi katika stendi ya mkoa wa Njombe wameiomba halmashauri ya mji huo kukarabati barabara zinazoelekea vijijini kutokana na kuharibika baada ya mvua kubwa kunyesha
Wakizungumza na mwandishi wetu madereva hao wamedai kuwa barabara nyingi zinazoelekea vijijini zimeharibika kitendo kinachopelekea kuchelewa kufika safari zao na hivyo kuonekana ni usumbufu kwa wateja wao ambao ni abiria
Nao baadhi ya abiria wamesema ubovu wa barabara hizo huwalazimu muda mwingine kushuka katika magari na kutembea kwa miguu
Ibrahimu Mkangala ni Mhandisi wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye amewataka watumiaji wa vyombo vya usafiri kuwa wavumilivu kwani halmashauri hiyo tayari imeshapanga mikakati ya kukarabati barabara hizo zilizoharibika mara tu mvua zitakapokwisha
Katika hatua nyingine mhandisi huyo ametolea ufafanuzi ukarabati wa stendi hiyo ya muda ya mabasi mkoani Njombe

from Blogger http://ift.tt/2nwl2WG
via IFTTT


Kategori

Kategori