Showing posts with label 2017 at 01:34PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:34PM. Show all posts
Kia..!!!menukaa CCM..Vigogo wengine Kibao Kumfuata Sophia Simb

Kia..!!!menukaa CCM..Vigogo wengine Kibao Kumfuata Sophia Simb

Baada ya kubadilisha katiba, CCM inaonekana kuendelea kujipanga kukabiliana na ongezeko la upinzani nchini baada ya kuteua makatibu wa mikoa na wilaya, wanaoelezewa kuwa “majemedari” waliopewa jukumu la kukipitisha chama katika mtihani wa kwanza wa uchaguzi wa ndani.
CCM inatarajia kuanza chaguzi za ngazi za chini za ndani wakati wowote kuanzia sasa na kukamilisha baadaye mwka huu itakapochagua wajumbe wa vyombo vya juu vya maamuzi.
Mtihani wa pili utakuwa uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa mwaka 2019 kabla ya kumalizia na Uchaguzi Mkuu 2020.
Ikiwa imetingishwa na Uchaguzi Mkuu uliopita, tayari CCM imeshapunguza idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu kutoka 34 hadi 24, na wa Halmashauri Kuu kutoka 388 hadi 160.
Imeondoa nafasi zisizo za kikatiba katika wilaya na jumuiya zake na kufanya mabadiliko ya sekretarieti. Na sasa imetangaza makatibu wa mikoa na wilaya.
“Hao ndio majemedari waliopewa jukumu la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mafanikio,” alisema kada mmoja ambaye hakupenda kutajwa jina lake.
Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM ilipoteza mawaziri wakuu wawili wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye ambao walifuatwa na makada wengine kadhaa wakiwemo wenyeviti wa mikoa, wilaya, wabunge na madiwani.
Pia CCM iliruhusu vyama vya upinzani, hasa vilivyokuwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupata zaidi ya viti 100 vya ubunge, viti zaidi vya udiwani na halmashauri 19.
Baadhi ya watendaji wa chama hicho hasa makatibu wa mkoa na wilaya, ndio wanaodaiwa kusababisha CCM kupata ushindi mdogo katika Uchaguzi Mkuu uliopita ambao ulikuwa na msisimko mkubwa.
Mwenyekiti John Magufuli alisema waziwazi kuwa makatibu hawakusaidia wakati wajumbe wa Halmashauri Kuu walipoimba wimbo wa kuwa na imani na Lowassa baada ya jina lake kukatwa na Kamati Kuu.
Hivyo, haikuwa ajabu kwa CCM kupanga upya safu ya uongozi kuondokana na masalia ya wasaliti, hasa wanaomuunga mkono Lowassa na wenzake.
Mapema wiki hii, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alitangaza majina mapya ya makatibu wa mikoa na wilaya. Kati yao wamo 31 wa mikoa na 155 wa wilaya. Hata hivyo majina yaliyotangazwa ni ya upande wa Bara pekee.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Polepole alisema uteuzi uliofanywa umezingatia weledi, jinsia na mpango wa kuachiana vijiti kwa kuzingatia rika.
Alisema kati ya makatibu hao walioteuliwa wa mikoa. kumi na moja ni wale waliopandishwa hadhi kutokana na utendaji wao, na 20 ni wapya kabisa.
Uteuzi huo umefanyika baada ya chama hicho kupitia ripoti ya tathmini ya uchaguzi uliopita na kubaini baadhi yao walikisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu na kusababisha kupoteza viti vingi vya ubunge, udiwani na baadhi ya halmashauri.
Uteuzi huo ni mwendelezo wa CCM kuweka majemedari wapya. Mwenyekiti alianza kupanga safu ya uongozi kwa kuwaondoa Rajab Luhwavi, aliyekuwa naibu katibu mkuu bara na nafasi yake kuchukuliwa na Rodrick Mpogolo, na Nape Nnauye, aliyekuwa katibu wa itikadi na Christopher Ole Sendeka akapewa usemaji wa chama.
Wengine walioondolewa ni Pindi Chana, aliyekuwa katibu wa NEC wa siasa na uhusiano wa kimataifa na nafasi yake kuchukuliwa na Kanali Ngemela Lubinga. Pia Vuai Ali Vuai, aliyekuwa naibu katibu mkuu Zanzibar, Dk Muhammad Seif Khatib na Zakhia Meghji. Nafasi ya kiutendaji ambayo haijaguswa ni ya katibu mkuu.
Makatibu hao kwa mujibu wa katiba ya CCM wana jukumu la kujua takwimu zote za chama katika maeneo yao ya kazi, ikiwamo idadi ya wanachama, matawi, mali za chama, kuandaa uchaguzi wa ndani na kufanya tathmini ya mgombea anayekubalika kwenye eneo lake.
Vigogo 12 wa chama hicho walifukuzwa uanachama kwa usaliti, akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba na wenyeviti wanne wa mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Shinyanga na Mara.

from Blogger http://ift.tt/2nNxWTH
via IFTTT


Majibu Kwa Diallo Kuhusu Alichojifunza Kwenye Sakata la Paul Makonda

Nimesoma andiko la Mbunge wa zamani wa Ilemela Mhe.Dr.Anthony Dialo kuhusu sakata la Makonda kuvamia studio za Clouds, kutetewa na JPM, Nape kuunda Kamati na yaliyomkuta Nappe baadae.
Katika taarifa hiyo ya Diallo anaeleza mambo kadhaa aliyojifunza kutokana na mikasa hiyo yote. Pamoja na mambo mengi anayodai amejifunza naorodhesha machache;
1. Amesema amejifunza kuwa Makonda ni kiongozi shupavu tangu akiwa Rais wa shirikisho la vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO). 2. Amesema amejifunza kuwa hakuna vyama vya upinzani Tanzania.
3. Anasema amejifunza vyama vya upinzani vimepoteza dira.
#MAJIBU:
1. Mhe.Diallo inaonekana anaongea vitu asivyovijua vizuri. Makonda hajawahi kuwa Rais wa shirikisho la vyuo vikuu Tanzania. However hakuna kitu kinachoitwa Shirikisho la vyuo vikuu Tanzania. Kuna Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania, ambayo kwa kifupi ndio TAHLISO. Na Makonda alikuwa Mwenyekiti sio Rais. TAHLISO haijawahi kuwa na kiongozi anayeitwa Rais. Msaidieni Diallo.
2. Diallo anasema hakuna upinzaninTanzania, halafu baadae anasema upinzani umepoteza dira. Kama upinzani haupo, huo uliopoteza dira umetoka wapi? Mbona anaongea na kujipinga mwenyewe? Msaidieni Diallo.
Huwezi kusema sina gari, halafu baadae useme gari yako imepasuka tairi. Kama huna gari hiyo iliyopasuka tairi imetoka wapi? Kuna haja ya somo la “Logic and argumentation skills” au “Critical Thinking” kuwa masomo ya lazima shuleni. Msaidieni Diallo.
3. Diallo anasema hakuna upinzani nchini wakati, aliyemgaragaza kwenye ubunge wa Ilemela mwaka 2010 na kumpoteza kwenye ramani ya siasa ni mpinzani. Highness Kiwia wa Chadema ndiye aliyemfanya Diallo mpaka leo yupo mtaani. Pengine angekua waziri muda huu, lakini Kiwia (mpinzani) akamng’oa kwenye ubunge. Leo anasema hamna upinzani?? Msaidieni Dialo.!!
By @malisa_gj
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2onEHc9
via IFTTT


Kategori

Kategori