ELIMU


HISTORIA YA KALE HADI FREEMASONS
KARATASI za kale za Wasumeria zinaeleza kwamba ANNUNAKI waliokuja na vyombo vieleavyo angani vyenye maumbile kama ya UNGO. Walikuwa ni kabila la MIJUSI au zaidi ya reptilia.

Wayahudi, wamelitaja hilo kama NEFILIM kwa maana ya watoto wa miungu au AWWIM; neon linalomaanisha viumbe watambaao kwa tumbo. Wafalme wa Misri mara zote wamekuwa wakihusishwa na NYOKA na REPTILIA.

Mtafiti mmoja wa Kimarekani DAVID SIELAFF anasisitiza kwamba NEFILIM sio watoto wa miungu bali ni kizazi baina ya binadamu na viumbe wasio kuwa binadamu baada ya mwingiliano wao.

BIBLIA ; kitabi kitakatifu cha Wakristo katika Agano la Kale, wavamizi hao wametajwa kama miungu. Wanadamu walipoanza kuongezeka katika nchi wasichana wao wakazaliwa, wana wa Mungu wakawaona wasichana wa wanadamu ni wazuri na wakawaoa yeyote kati yao… Mwanzo 6:1-4.
 Wachunguzi wengi wa mambo kuhusiana na kabila hilo la reptilia wanakubaliana kwamba wametokea katika nyota ya DRACO, iliyopo baina ya nyota saba zing’arazo sana na ambazo katika majina  mengi yajulikanayo kwanza moja ni GREAT BEAR (dubu kubwa); ile iliyopo kushoto mwa nyota hizo ni yaani kadubu kadogo (LITTLE BEAR) au NORTHERN BEAR (yaani ALFA)
  1. Mapiramidi ya Misri
  2. Sphinx-Sanamu la Simba lenye kichwa cha binadamu liliko eneo Gaza ambalo ni la zamani zaidi kuliko mapiramidi yenyewe.
  3. Sanamu la Angkor Wat-Hili lipo Kambodia na mengine kama hayo  nchini JAPAN
YALIYOJENGWA kwa ustadi mkubwa wa ELIMU YA NYOTA, elimu ya maumbo na sayansi ya hali ya juu yaani ASTRONOMY, GEOMETRY na SCIENCE.

Aidha yamejengwa moja kwa moja kwa kufuata uelekeo wa DRACO. Hata hivyo wachunguzi wengeine pia wa mambo wanadai kwamba kabila hilo la Reptilia, liliishi katika mashimo na mapango na inawezekana ndipo walipotokea.