Elimtaa na ujasiliamali: MAMA SELINA PART II


 KUTOKA ILE YA KWANZA (PART I)


Mgoga hii aina ya Mlenda inapendwa sana na kabila la waruguru kwa sababu inaleta sana hamu ya kula hasa hasa kwa wagonjwa na walio wazima.

Selina alisema kuwa mboga hiyo ikisha sindikwa huwa inasagwa na kuchekechwa na kisha kuwa unga kabla ya kupikwa.

Alisem,a baada ya kuolewa mwaka 1983 hakuona sababu ya kuendelea kukaa tu nyumba bila kujishughulisha, na ndipo alipo amua kuanza kutafuta maisha yake ya kujitegemea.

Alisema kuwa kabla ya kupata mafunzo ya kutengeza sabuni na batiki 1990, alianza na kazi ya kulima bustani za mbogamboga ili kujikimu kimaisha.

Baada ya miaka saba ya ukulima ndipo serina alip[o jitosa rasmi katika biashara ya kutengeneza batiki kwa kuanzia na mtaji wa shilingi 16,000.

Alisema kuwa kabla ya kuanza kutengeneza batiki alitumwa na kanisa la Moravian ofisi ya wilaya mkoani Rukwa, iliyo kuwa chini ya uongozi wa mchungaji Kibona na kamati yake kwenda kusomea utengenezaji wa batiki kwenye jingo la mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Selina aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki mbili ndipo alipo ludi rasmi kanisani , na kuanza kutoa mafunzo kwa akinamama, wakinababa, na vijana wa madhehebu mbalimbali.

ITAENDELEA BOFYA HAPA PART III