Msanii Bobi Wine ashinda ubunge nchini Uganda

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu kama, Bobi Wine ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo nchini humo.
Bobi Wine mwenye suti katikati akikabiliana na Askari Polisi mapema wiki hii
Wine, ambaye aliwania kama mgombea huru, aliwashinda wagombea wenzake wanne katika jimbo la Kyadondo Mashariki mwa Uganda kwa ushindi wa kura 25,659 kati ya kura elfu 33,310 zilizopigwa.
Kwa mujibu wa Gazeti la New Vision la nchini humo limeeleza kuwa baada ya kutangazwa Gazeti hilo linasema baada ya kutangazwa kuwa mshindi, aliahidi kurudisha umoja na mshikamano jimboni humo.
“Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki…Ninataka siasa zitulete pamoja… jinsi muziki ufanyavyo.“amesema Bob Wine.
Mwanamuziki huyo mapema wiki hii alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa muda kabla ya kuachiwa huru.
Kiti hicho cha ubunge kiliachwa wazi baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDC Kizza Besigye amempongeza mwanamuziki huyo kwenye kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Congratulations to Uganda NETBALL!! Winning by defiance-against heavy odds. She Cranes Are African Netball Champions https://t.co/PbLgW1YUES
— Kifefe Kizza-Besigye (@kizzabesigye1) June 30, 2017
Bobi Wine alianza muziki mapema miaka ya 2000 kabla ya kujitosa kwenye siasa uchaguzi mkuu mwaka 2016 na ngoma ambayo ilimfanya ajizolee umaarufu nchini humo ni wimbo wake wa Situka.
Kwenye wimbo huo, anatoa wito kwa raia wa Uganda kuchangia katika vita dhidi ya rushwa na ukiukaji wa haki nchini mwao.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tAB89x
via IFTTT