Askari Aliyeuawa Aacha Mke Anayetarajia Kujifungua..!!!

.Ayoub Mwaikambo, askari aliyeuawa katika shambulio dhidi ya gari la Jeshi la Polisi wilayani Kibiti, ameacha mke ambaye anatarajiwa kujifungua mwezi mmoja ujao.
Hayo yamebainika katika hafla ya kuaga miili ya askari nane waliouawa katika shambulio lililotokea Alhamisi jioni, huku kukiwa na taarifa nyingine ya kushambuliwa kwa mapanga kwa mtoto wa mwenyekiti wa Kijiji cha Kitembo wilayani Kibiti ambako mauaji dhidi ya viongozi na askari yanazidi kuongezeka.
Mtoto huyo, Saidi Abdallah alijeruhiwa kwa mapanga baada ya kukataa kuwatajia watu waliovamia nyumba yao usiku wa kuamkia jana, sehemu aliyojificha baba yake ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho.
Jana, wakati wa hafla ya kuaga miili ya askari hao iliyofanyika Kurasini Barracks, Francisco Mwaikambo, ambaye ni kaka wa askari huyo, alisema amempoteza mtu ambaye alikuwa akijadiliana naye mambo ya familia.
“Ah! Ayoub amekufa wakati nilikuwa nimepata mtu mwingine wa kujadiliana naye mambo ya familia baada ya kukua na kufahamu umuhimu wa familia,” alisema Francisco huku midomo ikimcheza mithili ya mtu anayejizuia kulia. “Amemuacha mtoto wake tumboni.”

from Blogger http://ift.tt/2p7wH3J
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2plJ9MS
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nRrHja
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nSgejK
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2pqPa8b
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oBwnqO
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oE8DDX
via IFTTT