HATUA ZACHUKULIWA KUHAKIKISHA KUWA RASILIMALI ZA UMMA ZINATUMIKA KAMA ZILIVYOKUSUDIWA KWA USTAWI WA MAENDELEO YA NCHI NA WANANCHI WAKE.


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa mbeya Ndugu Nicolausi Ntangu akifungua  semina ya wadau wa ukaguzi wa ndani  kanda ya nyanda za juu kusini iliyo fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mkapa. jijini Mbeya
Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Msaidizi Ndugu Chotto Sendo amesema semina hiyo ni sehemu ya mkakati wa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa serikali wa kuimalisha  mfumo wa uwajibikaji  na utawala bora katika matumizi  ya rasilimali za umma chini ya program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma awamu ya nne( PFMRP IV).
Wadau wa ukaguzi wa ndani kanda ya nyanda za juu kusini wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufngunguzi wa warsha hiyo
Mkaguzi wa ndani wa wa serikali msaidzi kitengo cha mshahara bajeti Sanslaus Mpembe akimshukuru mgeni rasmi kwa ufunguzi wa semina hiyo
Afisa habari Alexander Lweikila akifafanua jambo wa wadau 
Picha ya pamoja



SERIKALI  imeendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kama zilivyokusudiwa kwa ustawi wa maendeleo ya nchi na wananchi wake.
Moja ya hatua ambazo serikali imechukua ni pamoja na kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa ndani mkuu wa serikali ambayo imepewa jukumu la kusimamia  ,kueindeleza  na kuboresha huduma zaukaguzi wa ndani katika serikali na kuwaendeleza kitaaluma wakaguzi wa ndani.
  
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa mbeya Ndugu Nicolausi Ntangu wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa ukaguzi wa ndani  kanda ya nyanda za juu kusini iliyo fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mkapa.
Kaimu Katibu Tawala huyo amesema kuwa ofisi ya mkaguzi wa ndani inasaidia kwa asilimia kubwa katika kusimamia utawala  bora hasa katika mamlaka za serikali mitaa.
Amesema pia idara hiyo imekuwa ikihusika mojakwamoja  katika usimamiaji na uwajibikaji  wa matumizi  bora ya rasilimali za umma kama inavyoshauriwa kupitia taarifa mbalimali za ukaguzi wa ndani hivyo dhana ya uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali umma kuwa  muhimu sana kwa utendaji wa serikali.
  
Hata hivyo Ntangu amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya vitendo vinavyo fanywa na baadhi ya watendaji katika halimashauri na menejmenti mbalimbali nchini ambao umekuwa ukiwakwamisha wakaguzi wa ndani katika kutekeleza majukumu yao .
Amesema kuwa nivyema vitendo hivyo vya ukandamizwaji kwa wakaguzi  wa ndani vikakoma kwa lengo la   kuhakikisha ukaguzi wa ndani unapewa rasilimali za kutosha na kupewa kipaumbele katika utendaji wao wa kazi za kila siku.
  
Pia katibu tawala huyo amefafanua kuwa ili kuhakikisha Idara za ukaguzi wa ndani zinafanya kazi zake kwa weledi nivema M ameya ,Wenyeviti wa halimashauri na Wenyeviti wa kamati za ukaguzi wa za halimashauri  kuhakikisha zinatoa fursa kwa wakaguzi hao wa ndani ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo katika usimamizi  wa rasilimali za nchi.
Hata hivyo  kwa upende wake Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Msaidizi Ndugu Chetto Sendo amesema semina hiyo ni sehemu ya mkakati wa Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa serikali wa kuimalisha  mfumo wa uwajibikaji  na utawala bora katika matumizi  ya rasilimali za umma chini ya program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma awamu ya nne( PFMRP IV).
Amesema semina hiyo pia itasaidia  kuamsha hamasa kwa watendaji wa halimashauri  kwa lengo la kuanza  kuona ukaguzi ndani kama kiungo muhimu katika utekelezaji wa majukumu kama kiungo muhimu katika utekelezaji wa majukumu na kufikia malengo.
Amesema semina hiyo inatalajiwa  kufanyika katika kanda zingine za kati ,kaskazini ,ziwa na mashariki  kwa kushirikisha makundi yote katika halimashari zitakazo husika.