WAANDISHI wa
habari mkoani Mbeya wametakiwa kujikita katika uandishi wa habari za kijinsia
na haki za wakinamama.
Rai hiyo
imetolewa na Mwezeshaji kutoka mtandao wa wanawake na jinsia (TGNP), Bi. Kenny Ngomuo wakati
akizungunza na baadhi ya waandishi wa habari katika semina shirikishi juu ya
uandishi wa habari za vijijini na kuondoa ukandamizi dhidi ya wanawake.
Bi Keny
amesema kuwa wanawake na wanaume waishio
pembezini wamekuwa wakikandamizwa na mfumo dume.
Amesema waandishi
wanatakiwa kulivalia njuga swala hilo ili kuikwamua jamii yetu na ukandamizaji
wa kijinsia na mfumo dume.
MRATIBU WA MASUALA YA HABARI NA MAHUSIANO WA TGNP BI. KENNY NGOMUO AKITOA UFAFANUZI WA MALENGO YA SEMINA KWA WANAHABARI.
WANAHABARI WAKIFUATILIA KWA UMAKINI SEMINA HIYO.
wapili kulia ni mmiliki wa Elimtaa Bw Furaha Eliab
WANAHABARI WAKIJADILIANA KATIKA VIKUNDI JUU YA MADA ZINAZOHUSU MFUMO DUME
MWANDISHI WA HABARI KUTOKA TBC NDUGU HOSEA CHEYO AKICHANGIA MADA KUHUSU MFUMO DUME.
MWANDISHI WA HABARI KUTOKA MWANANCHI NDUGU STEFANO SIMBEYE AKIWASILISHA MADA YA KIKUNDI CHAKE KATIKA SEMINA HIYO
MRATIBU
WA MASUALA YA HABARI NA MAHUSIANO WA TGNP BI. KENNY NGOMUO AKISISITIZA
JAMBO KATIKA ILANI YA MADAI YA WANAWAKE WA TANZANIA KUHUSU KATIBA MPYA.
MRATIBU WA MASUALA YA HABARI NA MAHUSIANO WA TGNP BI. KENNY NGOMUO, AKIFUTILIA MJADALA WA WAANDISHI WA HABARI.
PICHA NA MBEYA YETU