WANANCHI WAOMBA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI

WANANCHI Mkoani Mbeya ameombwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi baada ya kupata ushirikiano na kufanikiwa kukamata siraha mbalimbali na sale zajeshi zilizo tumika katika matukio ya uporaji.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alisema kuwa kuwa kushilikia na wananchi wa Mkoani hapa wamefanikiwa kukamata silaha pamoja na sale za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) zilizo kuwa zikitumiwa katika matukio ya ujambazi.

Alisema jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha tano zilizo tumika katika matukio uporaji na ujambazi zikiwa na risasi.

Alisema risasi zilizo kamatwa ni za SMG/SAR 31, S/Gun 99, 25 za Bastoraamzabo zilikutwa katika magari ya majambazi hao ambapo zilikamatwa baada ya Jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa wananchi.

 Kamanda Athuman alisema kuwa sare hizo za JWTZ zilikuwa zikitumika kuwaazima majambazi ambao walikuwa wakifanya uharifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu wa Mbeya ikiwa ni pamoja na tukio la Chunya ambapo askali mmoja wa jeshi hilo kuuwawa.

Alisema Jeshihilo lilizikamata sare ambazo ni suruali na mashati manne, Kofia tatu na viatu (buti) jozi mbili ambavyo vilikutwa ndani ya gari la Gati Mbilinyi na nyumbani kwa Hilary Ng’ang’ana ambao ni kati ya majambazi walio kamatwa na jeshi hilo.

Jeshi hilo pia limekamata pia magari Saba ambayo yalikuwa yakitumika na majambazi katika matukuo hayo ambayo yalitowesha amani kuwa ni Toyota Corola, Noah, Vitz, Toyota Pick Up, Toyota Primio na Mark II,  zote zikiwa mali za watuhumiwa wa ujambazi.

Alisema anaomba wananchi kuendelea kutoka ushirikiano kwa jeshi hilo na kuataka wafiki katika ofisi za jeshi hilo mara kwa mara ili kutamua vitu vyao vilivyopo katika ofisi za jeshi hilo.