MKUU wa wilaya ya Mbarali Gulahamhussen
Kifu amewataka wakazi wa halmashauri hiyo kuondoa hofu kutokana na Dege ndogo
itakayo anza kuzuguka ikipima madini.
Ndege hiyo itakuwa ikipita karibu
sana na ardhi
kwa umbali wa mta 40 na kuwa itakuwa ikifanya upimaji wa madini katika
halmashauri hiyo.
Akizungumza na madiwani wa
halmashauri ya Mbarali juzi Mkuu huyo wa wilaya, alsema kuwa kuna kunandege
itakayo pita katika halmashauri hiyo ikifanya upimaji wa madini.
Alisema kuwa ndege hiyo itaanza
kuzunguka katika halmashauri hiyo hivikalibuni na wananchui wasiwe na wasiwasi
juu ya Ndege hiyo itakayo pita chini zaidi.
“Natoa wito kwa wakazi wa wilaya
ya mbarali kuwa msiwe na hofu juu ya ndege itakayo anza kupita hivi karibuni na
kuzunguka itakuwa inafanya utafiti wa madini hivyo msiwe na wasiwasi juu ya
ndege hiyo,” alisema Kifu na kuongeza.
“Ndege hiyo itakuwa ikifanya
upimaji wa madini katika maeneo yetu na itapita chini zaidi umbari wa mita 40
hivyo madiwani muwatoe hofu wananchi kuwapo kwa ndege hiyo.”
Alisema kuwa suala hilo watu wa ulinzi na
usalama, wilaya na mkoa wanalifahamu na kuwa hivyo ndege hiyo itakuwa salama na
wananchi usiwe na hofu kuhusiana na usalama wenu.