WAKURUGENZI na watumishi wa
halmashauri ya Mbarali wametkiwa kusimamia kwa makini ujenzi wa vumba vya
madarasa ili wanafunzi ambao wanahitajika kuingia madarasani waanze kusoma.
Akizungumza na madiwani wa
Halmashauri ya Mbarali katika Kikao cha baraza la madiwani, Mkuu wa wilaya hiyo
Gulahamsein Kifu alisema kuwa watumishi wasimamie kwa makini ujenzi wa vivyumba
vya madarasa.
Alisema madiwani wanawajibu
mkubwa wa kuwahimiza wananchi kuchangia nguvu ya serikali katika ujenzi wa
vyumba vya madarasa ambapo kuna wanafunzi wengi wanahitaji kuingia madarasani.
Alisema kuwa ni vema madarasa yakakamilika mapema ili
wanafunzi waanze mapema kuingia katika msimu huu wa masomo, na kuhakikisha
halmashauri haiingii katika aibu ya kumaliza mwaka kwa kuwaacha wanafunzi walio
fauli mtaa.
“Maafisa watendaji, madiwani
hakikiseni mnapanbana kukabiliana na kuwapo kwa upungufu wa madarasa katika
kata zenu na kuhakikisha wanafunzi waliofauru wanaanza masomo kwa wakati,”
alisema Kifu.
Aidha Kifu alimtaka mkurugenzi wa halmashauri
hiyo kufuatilia kwa ukalibu maendeleo ya ujezi wa madarasa na kuwahimiza
watendaji kufanya ujenzi huo wa kumaliza uhitaji huo.
“Mkurugezi unatakiwa kufuatilia
maendeleo na kunima mwendelezo wa ujenzi wa madarasa na sio mimi ndio
nifuatilie halafu nikueleza kinacho endelea katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa” aliongeza Kifu.
Kwa upande wake afisa elimu ya
sekondari wa halmashauri hiyo Claudia Kita alisema kuwa kuna vyumba 19
vinaendelea kujengwa na vyumba 25 vinahitajika kujengwa katika halmashauri ya
Mbarali.