Utalii Nchini Tanzania

BARIDI NJOMBE NA MAKAMBAKO HADI UKUNGU

Tembea Tanzania Njombe baridi cold
 Hali ya hewa ni moja ya vitu ambavyo hupelekea watu kusafiri toka eneo moja kwenda jingine kwa lengo la kukwepa hali flani au kuifuata hali ya hewa ya namna fulani. Kwa nchi nyingi za magharibi, watu wengi hupenda kusafiri mbali na wanapoishi ifikiapo kipindi cha majira ya joto. na baadhi yao hufanya hivyo kipindi cha baridi kali. Hali ya hewa ni kipengele muhimu kukifahamu unapopanga safari yako kwenda eneo flani hususan safari ya mapumziko. hali ya hewa inaweza kukulazimisha kutofanya shughuli ambazo ungependelea. mathalan, eneo linapokuwa lipo ktk kipindi cha mvua, shughuli zinazohusisha matembezi zinakuwa ngumu kuzifanya. ufikapo msimu wa baridi, maeneo mengine huwa na baridi kali kiasi cha kufanya maisha kuwa kero badala ya mapumziko kwa wewe usiyeizoea hali ya pale.
Tembea Tanzania Njombe baridi cold
 Kwa hapa Tanzania, maeneo ya nyanda za juu kusini yanafahamika kwa kuwa na baridi kali. hali iliyopeleka mpaka wajanja kuliita baridi 'Mufindi' - moja ya maeneo yaliyopo nyanda hizo. Hivi majuzi  nikiwa njiani kurudi dar mida ya asubuhi tulipita maeneo ya Njombe na makambako tukitokea mkoani Ruvuma. Mtundiko huu una baadhi ya picha nilizobahatika kupiga tukiwa njiani maeneo ya Njombe hadi Makambako ambapo tulikutana na ukungu mzito. Kuna sehemu ukungu ulikuwa ni mwingi kiasi cha kutulazimisha kupunguza mwendo kasi kwa kiasi kikubwa na kuwasha indicator za hazard kuepusha maafa ya namna yoyote ile.picha ya kwanza na ya pili ni maeneo kabla ya kufika Njombe Mjini ukiwa unatokea Songea.

KWA UFUPI NI HAYO TU Bofya hapa kwa mengi zaidi

MBUGA

Taswira Maridhawa - Mikumi National Park

Mikumi National Park Tembea Tanzania

 Mikumi National Park Tembea Tanzania

Mikumi National Park Tembea Tanzania

Mikumi National Park Tembea Tanzania

Mikumi National Park Tembea Tanzania

Mikumi National Park Tembea Tanzania

Mikumi National Park Tembea Tanzania